
Waziri Simbachawene aliwalalamikia maafisa elimu mikoa na wilaya kwa kuisababishia serikali madeni kwa watuimishi wake yasiyo ya lazima baada ya kuonekana kuwa walimu wengine wanawahamisha vituo vya kazi bila kuwa na sababu maalum na za msingi.
Wengi wao wamekuwa wakiahamishwa kazi kutokana na wivu wa maendeleo ya kimaisha na mafanikio au migogoro yta kiofisi ktk vituo vya kazi ambavyo wanafanya vitu ambavyo vinaweza kusuluhishwa kwa njai za kawaida bila kuhamishwa na kuisha.
Wakati fulani uhamisho unaweza kutolewa kwa mtu kwa kusudio la kumkomoa baada ya kuona kuna mgongano wa kimaslahi au kutoelewana na kukubaliana ktk mambo mengine na kujikuta wakiingiza serikali ktk madeni makubwa marakwa mara yasiyo ya lazima.
0 Comments "MAAFISA ELIMU MIKOA,WILAYA WAAGIZWA KULIPA MADENI YA WALIMU WALIOPEWA UHAMISHO"