ALIYETISHIA BASTOLA HADHARANI AWEKWA KIKAANGONI

Siku ya machi 23 Mh.Moses Nape Nnauye aliandaa kufanya mkutano  na waandishi wa habari ktk hoteli ya protea na kushindikana kufanya kama ilvyokusudiwa kui gia ukumbi maalum ulioandiliwa kwa ajili ya shughuli hiyo baada ya maafisa usalama wengi kuja na kuzuia tukio hilo lisifanyika kabisa.

Maafisa hao wa usalam ambao walikuwa ktk mavazi ya kawaida ya kiraia walifika eneo hilo nakumzuia Nape kushuka kutoka ndani ya gari yake ili kufanya mkutano huo hata kwa kuwahutubia waandishi nwa habari eneo hilo la barabarani.

Alijitokeza afisa usalama mmoja aliyevalia suruali ya jinzi ya bluunna shati yenye mistari ya bluu kwa mbali pia huku kichwani akiwa amevalia kofia maarufu kama kapelo na kuanza kumsukuma Mh.Nape Nauye kurudi ndani ya gari alikotoka lakini Nape alibisha juu ya Tukio hilo ndipo Jamaa huyo aliamua kuchomoa bunduki ndogo(bastola) iliyokuwa kiunoni mkono wa kushoto na kumtishia Mh.Nape Nnauye kurudi ndani.

Nape alililalamika sana juu ya swala hili la kuitishiwa amani mbele ya hadhara na vyombo vya habari ni kitu cha kustaajabisha kabisa.

Hali hiyo ya ajabu kufanyiwa kiongozi wa ngazi za juu wa serikali tena mbele ya umma imekosolewa na wanaharakati wengi wa haki za kibinadamu,wananchi na hata viongozi wengi wa serikali wa ngazi za juu  kuwa endepo mambo hayo yataachiwa kuendelea basi tutaiweka nchi hatarini.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Dar es salaam Simon sillo na IGP Ernest Mangu kuingilia kati tukio hilo na kumapa adhabu stahiki kachelo huyu aliyekiuka miiko ya kazi yake mbele ya macho ya uma wa watanzania.



Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "ALIYETISHIA BASTOLA HADHARANI AWEKWA KIKAANGONI"

Back To Top