MBUNGE WA ZAMANI MTWARA MJINI AONYESHA UKADA WAKE WA DAMU KWA KUTOA USAFIRI WA BURE

Inaweza kuwa ajabu sana kwa miongoni mwetu kufukia hatua ya kukufanyia mabaya kisha wewe ukamlipa mema.

Hali hii isiyo ya kawaida imetokea leo  eneo la  mtwara Mjini  baada ya mbunge wa zamani ajulikane kama (Murji) maarufu anajulikana kwa kumiliki maduka na kampuni kubwa yabusafirishaji ya Machinga kwa mikoa ya kusini.

Kampuni hii ya machinga inayofanya kazi ya kusafirisha miazigo na abiria kwenda Dar es salaam,Pwani,Lindi Masasi na maeneo ya mikoa mingine.

Imekuwa ni  kawaida kwa mbunge huyo  wa zamani mwenye asili ya kihindi kutoa usafiri ktk sherehe za ndoa,misiba,kusafirisha wanafunzi kwenda shule ba kurudi,shughuli za chama kwa wapiga kura wake wakati alipokuwa mbunge.

Ktk Uchaguzi wa mwaka 2015 Mbunge huyu aliangushwa na chama cha CUF kwa kuchaguliwa kwa mbunge Maftaa Nachuma kwa tiketi ya chama hiko.

Ajabu ya mbunge huyu wa zamani imezidi kuonekana ktk ziara ya Rais Magufuli ktk mkoa wa mtwara kwa kuonekana kuendelea kusitisha Gari zake nyingi kufanya biashara kwa Sikh mbili hizi na kufanya kazi ya kubeba raia  ktk kila aneo ambalo Rais  anatembelea.

Hii inaweza kuwa picha au viashilia vya kuwa mbunge huyu wa zamani bado analitamani sana jumbo lake mtwara Mjini hivyo anatengeneza mbinu kulikwaa tena.

Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme

Related Post:

0 Comments "MBUNGE WA ZAMANI MTWARA MJINI AONYESHA UKADA WAKE WA DAMU KWA KUTOA USAFIRI WA BURE"

Back To Top