Rais John Joseph Magufuli akiwa ktk ziara yake kwa mikoa ya Pwani,Lindi na Mtwara wiki hii,Leo tarehe 4 asubuhi hii akiwa ktk ufunguzi wa kiwanda cha dangote kilichopo nje kidogo ya mji wa mtwara amehutubia mamia ya wananchi na mwishoni kabisa madereva walikua na yao ya kusema.
Mwakilishi wa wafanyakazi madereva ktk kiwanda hiko alipita mbele ya rais Magufuli na kutoa malalamiko yao juu ya kiwanda hiko yaliondaliwa ktk kurasa kadhaa.
Dereva huyo akiwakilisha matatizo ya madereva wenziwe na wafanyakazi wote kwa ujumla alianza na malalamiko juu ya ajira zao licha ya magari zaidi ya 600 kuletwa mwishoni 2016 kwa ajili ya shughuli za kiwanda hiko kukaa bure bila kutumika kwa miezi yote hiyo bila taarifa yeypte licha usahili ulifanyika na baadhi ya kufuzu Ila mpaka Leo hawajaanza kazi badala yake gari binafsi 200 zunazomilikiwa na wahindi kuendelea kufanya kazi hiyo kwa mda wote.
Pia mwakilishi huyo alilalamikia juubya uwepo wa zaidi ya wahindi 100 kama raia wa kigeni kufanya kazi ambazo watanzania wangeweza kuzifanya,alihoji uhalili wao.
Pia aliongeza kuwa kuna mambo mengi yanayoendelea ndani ya kiwanda hiko ambayo ni hatari kwa maendeleo ya ajira na wafanyakazi kiujumla na yatarudisha juhudi za za mh. Rais Magufuli endapo yataachwa kuendelea.
Rais Magufuli alimaliza kwa kukubali maombi yao na aliaguza nakala apewe Dangote kama mmiliki wa kiwanda na nakala nyingine apewe yeye na kuahudi kushughulikia matatizo yao.
0 Comments "JIPU KUU LATUMBULIWA MBELE YA JPM DANGOTE"