Wengi wetu hatuna ugeni na taarifa juu ya kilichotokea ofisi za clouds media zilizopo eneo la mikocheni jijini Dar es salaam,Siku ya ijumaa usiku majira ya saa nne usiku ktk studio za clouds media kumeripotiwa juu ya tukio la mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bw.Paul makonda kuingia eneo hilo akiwa na Kundi la polisi wapatao sita wakiwa na bunduki.Hatua hii iliwastua watu wote wa eneo hilo haswa mlinzi wa getini licha ya kuwa sio mara ya kwanza kwenda hapo,kwani amekuwa na tabia ya kwenda ktk studio hizo za redio na runinga kwa ajili ya kufanya vipindi mbalimbali vya redio na runinga ambavyo anaalikwa kuhudhuria.
Lakini siku hiyo ilikuwa tofauti kwanza kwa mda alifika ofisini hapo lakini pia na kundi kubwa la polisi wenye silaha za bunduki ilionekana wazi siku hiyo haikuwa ya amani kama ilivyozoeleka siku zote kwa kiongozi huyo anakuja wakati mwingine hata kwa ajili ya kutembelea na kushinda hata kama hajaitwa.
Ukaribu huo wa mkuu wa mkoa huyo ulitokana na kuwa na urafiki na mmiliki wa clouds media Bwana Joseph Kusaga na Bwana Ruge Mutahaba ambaye ni Maneja wa clouds media yenye wafanyakazi zaidi ya 200.
Kikubwa ktk sakata hilo ni juu ya uvamizi wa kundi hilo la askari wenye silaha wakiwa wameongozana na Bw.Paul Makonda waliingia kwa kutumia nguvu hadi ndani ya ofisi hizo na kulazimisha juu ya kurushwa kwa kipande cha video ya mama aliye rikodiwa juu ya kuwa na mauhusiano na kuzaa na mchangaji Josephat Gwajima wa Kanisa la ufufuo.
Video na picha hizo zilizoenea mitandaoni zaidi ya wiki nzima iliyopita juu ya kumuonyesha mama huyo akiwa amebeba mtoto mgongoni akihusishwa Gwajima juu ya uhusiano na mtoto huyo ndio iliyoleta kashkash nzima kwa mkuu huyo kwenda kutaka kurusha ktk kipindi cha SHILAWADU kinachoendeshwa na Sud brown,Chris na Kwisa na kushindwa kufanya hivyo ndipo mkuu wa mkoa huyo aliamua kwenda studio hizo na kufanya fujo nyingi.
Clouds media leo kupitia Meneja wa clouds bwana Ruge mutahaba ametoa maelezo juu ya sakata kwa kusema sababu ya kukataa kurusha habari hiyo ni juu ya kutokuwa na upande wa pili yaani maelezo ya Josephat Gwajima hivyo kwa sheria za habari ni kosa kubwa kurusha taarifa ktk vyombo vya habari ambayo haina uhakika na haina mizani yaani haina maelezo ya pande mbili.
Taarifa za chinichini siku ya uvamizi kuwa Mkuu huyo aliingia Ndani na kulazimishwa kupewa Dvd iliyokuwa na vipande vya mwanamama huyo mwenye kushutumiwa juu ya kuzalishwa na askofu Gwajima.
Tukio hili la uvamizi huo wa ofisi za clouds media limeongelewa kwa kirefu sana na meneja wa clouds Bw. Ruge Mutahaba.

0 Comments "KILICHOTOKEA OFISI ZA CLOUDS MEDIA NI AIBU,KINASIKITISHA NA KUSHANGAZA WATU."