JPM:KUFIKA MTWARA KUFUNGUA BENKI KUU KANDA YA KUSINI

Rais John Pombe Joseph Magufuli leo terehe 3 yupo mkoani lindi akiwa na ziara ya siku mbili kuanzia jana alipoingia ktk mkoa huo akitokea Dar es salaam  kupitia mkoa wa pwani na kuzungumza na wananchi wa miji ya njiani kama Mkuranga,Ikwiriri
Na alipofika Somanga mkoani lindi aliwaacha hoi wananchi wa mji huo pale alipowambia kuwa wanalalamika kuhusu njaa wajitahidi kulima kwa bidii kwani vyeginevyo  watakufa kwa njaa kwa uzembe kwani mvua zinanyesha na ardhi iko vizuri.

Kesho tarehe 4 Rais magufuli atafika mkoani mtwara na kupokelewa na mkuu wa mkoa mtwara Bi Halima Dengego na atakua hapa kwa siku mbili na kufungua jengo la benki kuu kanda ya kusini lililopo mtwara mjini,pia Rais Magufuli atakwenda bandari ya mtwara kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa kutengeneza gati mpya.

Bandari ya mtwara ndio bandari yenye kina kirefu kuliko zote nchini na hivyo kuwa nauwezo wa kuruhusu kuingiza meli kubwa na mizigo mikubwa.

Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme

Related Post:

0 Comments "JPM:KUFIKA MTWARA KUFUNGUA BENKI KUU KANDA YA KUSINI"

Back To Top