HATIMAYE TANZANIA KUWAPA KENYA MADAKTARI 500

Kuna msemo usemao kuwa "vita ya nzige furaha ya kunguru" kutokana na mgogoro wa madaktari nchini kenya uliodumu zaidi ya miezi mitatu na kulazimu Rais wa kenya Uhuru kenyatta kutangaza kwa madaktari hao kuwa endapo wataendelea zaidi nna mgomo huo basi serikali yake itaamua kuwafukuza madaktari hao kazi na kuwaajili wengine kutoka Tanzania na cuba.

Waziri wa afya wa kenya Bw. James macharia leo alikutana na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa ajili ya kuwasilisha ombi lake la kuhitaji madaktari zaidi ya 500 kwa awamu ya kwanza.

Waziri wa afya wa Tanzania Mh.Ummi Mwalimu aliongeza kuwa masharti ya madaktari wanaotakiwa kuomba kazin hiyo ni asiwe mwajiliwa serikalini,awe amefanya mafunzo ya vitendo zaidi ya miaka miwili pia awe amesajiliwa na chama cha madaktari nchini.

Mh.ummi mwalimu aliongeza kuwa madaktari hao watalipwa stahiki zao zote ikiwemo mshahara,nyumba na posho zao zote kwa mfumo wa dola,serikali ya kenya imeahidi kulinda usalama wao kwani hata hivyo uendaji wao hausiani na mgomo wa kenya bari kutokana na upungufu wa madaktari nchini humo.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "HATIMAYE TANZANIA KUWAPA KENYA MADAKTARI 500"

Back To Top