YOWERI KAGUTA MUSEVEN AIWEKA UGANDA KIGANJANI

Siku moja toka kuwasili nchini kwa Rais wa Jamhuri ya watu wa uganda Mh.Yoweri Kaguta Museven kwa ziara ya kikazi kwa mwenyeji wake Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.John Pombe Joseph Magufuli kuja kuzungumzia mambo mbalimbali yanayohusu nchi zao ikiwemo uchumi,bomba la mafuta,ushirikiano wa kiviwanda,kidiplomasia.
Ikumbukwe kuwa nchi ya Uganda ni miiongoni mwa mataifa yalikuwa na shida ktk utawala kwani kumekuwa na kupinduana ktk madaraka toka miaka ya 1970,uganda ilipata uhuru wake toka kwa waingereza mwaka 1962 na kuwekwa edward mutesa 2 kufuatiwa na apollo milton obote kisha kuja kupinduliwa kijeshi na aliyekuwa mkuu wake wa Majeshi Idd Amin Dada mwaka 1971 na kuitwala kidikteta nchi hiyo hadi pale majeshi ya Tanzania yalipokwenda kuivamia mwaka 1978 na kumpiga Idd Amin na kukimbilia Saud arabia mpaka kifo kilipomkuta.

Baada ya hapo nchi ilitawaliwa na rais wa mpito bwana Yusuph kironde Lule kwa mda wa miezi miwili tu na baadae kutawaliwa Godfrey lukongwa binaisa 1979-1980,kisha urusi kwa Apollo milton obote 1980-1985,Tito okello luswa 1985-1986 kwa miezi kadhaa tu na kuja kupinduliwa na kiongozi wa waasi wa msituni bwana Yoweri kaguta museveni.

Yoweri Kaguta Museven alizaliwa 15/8/1944 huko Ntungamo uganda kwasasa ana umri wa miaka 72,mkewe Janeth museven alioa mwaka 1973 amefanikiwa kuwa na watoto wanne.

Museven aliingia madarakani 29/1/1986 na kufanikiwa kuitawala Uganda hadi sasa licha ya kuwepo mgawanyiko wa kimakabila na vikwazo vya kisiasa na kutoka kwa mpinzani wake mkuu Bwana Kizza Besigye,museveni amelaumiwa ndani ndani na nnje ya nchi yake kwa kuonekana kukikandamiza demokrasia na wapinzani kwa ujumla kwa kibadili katiba ya nchi hiyo mara kadhaa ili kupata nafasi ya kutawala taifa hilo.

Museven pia amesifika kwa kuthibiti vikundi vya waasi vya kaskazini mwa uganda vilivyoongozwa na Joseph kony,pia kuyaweka makabila yote pamoja haswa kabila kubwa lenye himaya zake la Baganda na kuwa na wafalme wake wa kimaeneo.

Nchi ya uganda inaonekana kutulia sana ktk mambo ya kisiasa na hata uchumi baada ya kukoma kwa mapinduzi ya serikali yaliokuwa yakifanywa mara kwa mara na majenerali wa kijeshi,mMuseven alichukua elimu yake ya juu ktk chuo kikuu cha Dar es salaam ktk kuchukua digrii ya uchumi,,amekuwa mpingaji wa maagizo ya hovyo kutoka nchi za magharibi na marekani kama yale ya kutaka kuwatambua mashoga.

Yoweri museven anafahamika kujenga nchi yake kiuchumi wa juu licha ya kuwa na changamoto kubwa za kifedha na kisiasa,kifupi ni mkongwe wa siasa ktk ukanda wa nchi zote za afrika mshariki na kati hivyo.

Ziara yake ya siku mili nchini inategemewa kuzaa matunda kwa watanzania akiwa na mwenyeji wake Mh.Joseph Magufuli.



 

Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme

Related Post:

0 Comments "YOWERI KAGUTA MUSEVEN AIWEKA UGANDA KIGANJANI"

Back To Top