WAZIRI MKUU AWASHA MOTO KIWANDA CHA MBOLEA MANYARA

Waziri mkuu Majaliwa kassim Majaliwa amekerwa na  hali ya kiwanda cha kuzalisha mbolea cha (minjingu) kilichopo mkoani manyara,Waziri mku ambaye yupo ktk ziara yake mkoani humo akiwa ameambatana na mkuu wa mkoa wa manyara  mh. Joel bendera,waziri wa kilimo na vuvi Dk. Charles Tizeba walifanya ziara hiyo ktk kiwanda cha kutengeneza mbolea ya kilimo maarufu kama minjingu kilichopo mkoani manyara.

Waziri mkuu hakuridhishwa na utendaji kazi wa kiwanda hiko pia zaidi alikerwa na kitendo cha kiwanda kutumia vifungashio vyenye nembo na anwani ya nchi ya kenya ambapo ndipo vinatengezwa. Vifungashio hivyo ambavyo ni viroba vilivyoandkwa(bungoma county nairobi mombasa kenya) kitendo hiko kilimuudhi waziri mkuu na kusema vitu vingi vinavyotengenezwa Tanzania vimekuwa vikipoteza uhalisia kwa kuwa na nembo na anwani za mataifa mengine hivya kuonekana kama vinatoka huko wakati ukweli vinatengenezwa Tanzania,mfano madini ya Tanzanite yanayopatikana Arusha pekee duniani kote sasa yanaonekana yanatoka afrika ya kusini na kenya.

Hali hii imemlazimu waziri mkuu kuamuru uongozi wa kiwanda hiko cha minjingu manyara kuandika barua maalum kujieleza kwanini imekuwa hivyo na ipelekwe kwa rais Dk John Pombe Magufuli na nakala moja ifikishwe ofisini kwake haraka.

Kitendo cha kutunia bidhaa za ndani zenye nembo ya nchi nyingine nin kupotosha uhalisia wa kauli ya kiongozi wetu mkuu Rais JPM anayetaka na kusisitiza Tanzania ya viwanda siku zote.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "WAZIRI MKUU AWASHA MOTO KIWANDA CHA MBOLEA MANYARA"

Back To Top