SAKATA LA WATANZANIA WALIOPO MSUMBIJI LAFIKIA PABAYA

Sekeseke linalofuka moshi nchi ya jirani ya msumbiji iliyopo kusini mwa Tanzania ikiwa inapakana na mkoa wa mtwara limefikia pabaya  baada ya balozi wa tanzania ktk nchi hiyo kutoa amri ya kuwataka watanzania wote waliopo msumbiji kurejea Tanzania ndani ya siku tano (5) tu.

Wiki hii ndani ya mkoa wa mtwara hasa kutoka mpakani ktk kijiji cha kilambo kumeshuhudiwa makundi kwa makundi ya watu wakitokea nchi hiyo wakiwa wamepakizwa ktk malori binafsi na ya jeshi na kuja kushushwa ktk viwanja vya mashujaa na nyumba za kulala wageni maarufu kama chilindima mtaa wa chikongola  mtwara mjini.

Hali ya wahamiaji hao wanaoitwa haramu huko msumbiji imekuwa tete sana kwa kurudishwa wakiwa wameacha mali,nyumba,wamepoteana na jamaa zao wa huko,kuwekwa vtuo vya polisi bila kula wala kunywa maji, wengi wao walikuwa wakiishi porini kukwepa ukamatwaji na kufanyiwa vitendo vya ubakaji na upigwaji na kunyanyaswa kijinsia.

Watu hao ambao wamekuwa wakiishi ktk viwanja vya mashujaa ambapo wamejengewa mahema,wamekuwa wakilalamika kuwa hali ya kimaisha imekuwa ngumu sana kwao kutokana na kukosekana kwa huduma za msingi kama chakula,maji,choo na kukosa faragha kwa wanaume na wanawake kuishi sehemu moja.

Hadi sasa hakuna taarifa na chanzo maalum kwanini watanzania wanatendewa hivyo ukiachana na kutokuwa na vibali maana wengi ya wanaorudishwa wanavyo vibali ila walipokamatwa vilichukuliwa pamoja na pesa,vitambulisho na hawakuvipata tena.

Baadhi ya watu wanasema kisa ni kufukuzwa na kunyanganywa kwa eneo la ardhi kwa tajiri mmoja wa msumbiji alilokuwa anamiliki huko mikindani anaejulikana kama Franco lakini pia wengine wanahisi ni tabia mbaya na vitendo vya uhalifu wanavyotenda watanzania kwa wenyeji pindi wanpokuwa huko msumbiji(wizi,ukabaji,uporaji,utapeli) pia ujanja wa watanzania ktk kuchangamkia fursa wakiwa huko na kuleta chuki kwa wanyeji dhidi ya wageni.

Hata hivyo magari ya jeshi yamefanya msaada wa kuwapeleka baadhi ya watu na kuwarudisha makwao kama mikoa ya Ruvuma,dar es salaam,lindi na pwani.

Taarifa za hivi punde kuwa viongozi wa serikali wamemuagiza balozi wa Tanzania nchini msumbiji kwenda kuuliza sababu za kuwarudisha na kuwapiga watanzania waliopo huko.


Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "SAKATA LA WATANZANIA WALIOPO MSUMBIJI LAFIKIA PABAYA"

Back To Top