MICHAEL JACKSON MWANAMZIKI TAJIRI,MACHACHALI NA ALIESUMBUA ULIMWENGU KABLA NA BAADA YA KIFO CHAKE

Unapohitaji kutoa historia ya mwanamuziki Michael jacckson huwezi kuwa na maneno ambayo unaweza ukaandika au kusimulia na ukamaliza mambo ambayo ameyafanya mwanamuziki huyu ktk maisha yake ya miaka aliyobahatika kuishi kuanzia 1958-2009 pale kifo kilipomkuta.

Sitokuwa na mengi ya kuandika kuhusu michael jackson bali nitatoa machache na ya msingi ambayo aliyafanya ktk uhai wake huo wa miaka 51 aliyobarikiwa kuishi hapa duniani.

Utakapokusanya kundi la watu mia moja(100) basi( 98) kati yao watakuwa wanazo taarifa juu ya michael jackson kutokana na umaarufu wake ktk fani ya mziki wa miondoko ya pop na kufuikia mahali kupewa jina la utani kama (king of the pop) yani mfalme wa mziki wa pop duniani.

Michael joseph jackson  ndio jina lake halisi na alizaliwa (29/8/1958) huko gary jimbo la indiana nchini marekani,michael yeye ni mmarekani mweusi mwenye asili ya afrika na alizaliwa ktk familia ya watoto watano yaani (michael,tito,jaermaine,marlon,brandon,jackie na dada yao janeth).

Baba yake anajulikana kama joe jackson na mama yake anaitwa Katherine jackson ambao walioana zaidi ya miaka 60 iliyopita huko nyuma.

Alioa mwanamke wa kwanza ajulikane kama Lisa marie preshey 1994 na kauachana nae 1996 na akaoa tena Debbie rowe mwaka 1996-1999 akamuacha,Michael alipata watoto kama pari,prince,jackson1,jackson2.


Michael alikuwa na kazi zifuatazo yaani kuimba,kutunga nyimbo,kucheza,kutengeneza mziki,kuigiza filamu,na uwanamitindo. Kipaji cha masanii huyu kilianza kuonekana mwaka 1964 pale walipounda kundi la mziki lilivuma sana kama The jackson five na laianza kuimba akiwa peke yake (solo) mwaka 1971 na kuja kufahamika zaisi miaka ya 1980. Yeye pia aliigiza filamu kama the wiz 1978 moon walker 1988,michael jack 2016

Ktk mwaka 1979 michael alitoa album yake iliyomtambulisha ktk ulimwengu wa mziki ilijulikana kama (off the wall 1979,thriler 1982,bad 1987,dangerous 1991,history 1995) albam ya Thriler iliuza zaid ya nakala milioni 65 na ndio iliuza kuliko albam zake zote.

 Nyimbo maarufu zilizomtambulisha ni kama be(beat it,billie jean,i just cant stop loving you,dirty diana na nyimbo aliotoa mwaka 2014 aliyoiita love never felt so good iliyongia kwenye chatin kubwa ya mziki marekani kama billiboard.

Maisha ya michael jackson yalitawaliwa mambo kama ya kutaka kubadili jinsi yake kuwa ya kike,alibadili rangi ya ngozi yake na kuwa kama mzungu,kuchonga pua,kubadili nywele na amaumbile yake mengi ya mwili.

Alikuwa mwanamuziki mwenye ujuzi wa hali ya juu nwa kuimba na kucheza mwenyewe kwa machachari sana anapiokuwa jukwaani,na alipata idadi kubwa ya watu walikua wanahudhuria matamasha yake sehemu mbalimbali duniani akipita kuchangisha pesa kusaidia watu wasiojiweza,yeye ndio mwanamuziki aliewweza kuanzisha mashirika zaidi  ya 39 ya kuasaidia watu amasikini na wenye matatizo.

Michael alipokea tuzo zaidi ya 13 za grammy awards na kuuza zaidi ya nakala milioni 350 nyimbo zake na kuapata mamia ya tuzo kutoka ktk mashirika mbalimbali ulimwenguni.

miongoni mwa kashfa kubwa alizowahi kupata ni juu ya kujibadili maumbile,kujihusisha na dini za kishetanui kwa =watu kuona aina ya video za miziki yake ambazo zilikuwa zikitisha sana kama thrilern.k.

Michael aliendelea kuimba na kushirikiana na wanamuziki mbalimbali ulimwenguni na kuendelea kufanya vizuri zaidi ktk mauzo na kampuni zake za  mtv,universal,sony ambazo zililkuwa zinarekodi nyimbo zake nyingi akiwa anasuimamiwa na joe jackson kama maneja wake ambae ni baba yake mzazi.

Kuna nayakati alikuwa akiumwa na kushindwa kuhudhuria baadhi ya matamasha na watu walihisi ni kutokana na athari za kubadili maumbile yake.

Utajiri alioacha michael jackson ni zaidi ya dola bilioni mbili kama thamani na ktk akaunti zake ameacha zaidi ya dola milioni mia nane 800 za kimarekani na anamiliki nyumba na majengo mengi ya kifahari sehemu nyingi za dunia na ndani ya marekani na hata huko afrika ya kusini.

Michael alikufa tarehe 25/6/2009 akiwa na umri wa miaka 51 huko holmbily hills los angeles calfornia marekani ktk jumba lake la kifahari. mali zake zote ziko chini ya himaya ya kaka yake mkubwa Jarmaine jackson.

Historia ya michael jackson kamwe haitofutika ktk ulimwengu wa mziki.










Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme

Related Post:

0 Comments "MICHAEL JACKSON MWANAMZIKI TAJIRI,MACHACHALI NA ALIESUMBUA ULIMWENGU KABLA NA BAADA YA KIFO CHAKE"

Back To Top