SABABU ZA WAJAWAZITO WENGI KUJIFUNGUA KWA NJIA YA UPASUAJI ZAANIKWA HADHARANI

Imekuwa jambo la kawaida  kwa watu kusikia ktk wanawake wajiwazito kumi walikwenda hospitali kwa ajili ya kujifungua basi sita wanajifungua kwa njia ya upasuaji au operesheni (operation).

Kujifungua kwa njia ya upasuaji ni njia mbadala ambayo utumika kwa mama mjazito pindi anapokuwa na dharura au matatizo ya kiafya yanayofanya kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida,sababu hizo zinaweza kuwa na njia ndogo,nyonga ndogo,kuwa na umri mdogo,kuwa na kiumbe kikubwa,magonjwa kama ya ukosefu wa damu,mtoto kugeuka au kukaa vibaya n.k

Njia za upasuaji ziko za aina mbili yaani kubwa ile ya kuchana sehemu ya chini ya tumbo (operesheni kubwa) na ile ya kuongeza njia ya uzazi kidogo(oporesheni ndogo).Idadi ya wajawazito wanaojifungua kwa njia hizo za operesheni imekuwa ikiongezeka kwa kasi kuliko zamani wataalam wa mambo ya afya wameweka wazi jambo hili;-

Ulaji wa vyakula vingi vya protini ambayo ufanya kiumbe kukua kwa haraka na kuwa mnene kuliko kawaida,kutokufanya mazoezi au kujishughulisha na kazi,kubeba mimba ktk umri mdogo au utotoni,kubeba mimba ktk umri mkubwa zaidi,kuomba wenyewe kufanyiwa hivyo kwa kuhaofia uchungu wa kuzaa,kuwa na nyoga ndogo za kutosha mtoto kupita,kukaa vibaya kwa mtoto ikiwemo na kutangulia miguu badala ya kichwa,kujisikia kuzaa au kujifungua kabla wakati maalum,kuwepo na fununu kuwa mtu anaejifungua kwa njia ya kawaida anaharibu maumbile ya ya siri au kutanuka zaidi.

Sababu nyingine ni za kiabiashara kutokana na wimbi kubwa la wajawazito wanaohitaji kujifungua kwa operesheni basi ya wahudumu wa afya wasio waaminifu wamekuwa wakitoza pesa hadi laki saba kwa tukio hilo,wengine waliokuwa na mchezo wa kufanya mapenzi kinyume na maumbile wanaogopa kuabika hivyo uamua kuzaa kwa operesheni,kutaka kupatan tarehe maalum kwa mtoto ajae.

Kifupi sababu ziko nyingi ila wengine wanawaza kuwa ni imani za kishirikina pia uchangia hii na wengine wazani ni kuacha mila na desturi,pia utumiaji wa njia za kuzuia mimba kama madawa,vijiti na sindano pia  uchangia hili.

Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme

Related Post:

0 Comments "SABABU ZA WAJAWAZITO WENGI KUJIFUNGUA KWA NJIA YA UPASUAJI ZAANIKWA HADHARANI"

Back To Top