WABUNGE WACHARUKA WATAKA MAKONDA AITWE NA KUHOJIWA



Mkutano unaoendelea asubuhi hii wa bunge Mjini Dodoma umekubwa na mijadala mkali kuhusu kuzungumzia swala la  Mkuu wa mkoa dar es salaam.
Mjadala huo umezungumzwa  na baadhi ya wabunge juu ya kauli za dharau kama kusema wabunge wanasinzia,hawafanyi kazi,ataashughulikia mmoja baada ya mwingine.
Mbunge halima mdee wa kawe,mbunge wa geita vijijini maarufu kama msukuma,zitto kabwe mbunge wa kigoma mjini na baadhi ya wabunge wengine wameongea kwa ukali na kukemea kauli hizo za kuwaona wabunge wapuuzi kama walivyodai.

Kutokana na mwenendo wa watumishi wa serikali kama wakuu wa mikoa,wilaya na wakurugenzi kuwadharau wabunge wanapokuwa ktk maeneo yao.

Binge limedhamilia kumuita Mkuu wa mkoa dar es salaam bungeni na kumuhoji juu ya tuhuma hiyo.
Kikao cha leo  kinachoendeshwa na mwenyekiti wa bunge  Mwanasheria Mkuu wa zamani wa serikali mh.Andrew chenge.

Sakata hilo  linatokana na ufuatiliaji wa madawa ya kulevya ambalo limeanzishwa na mkuu wa mkoa wa dar es salam.

Wabunge pia wamekosoa swala la kiongozi wa nchi kupiga simu hadharani na kuongea ikiwa kwa sauti ya juu kitu ambacho wao wanaona ni udhalilishaji kwa kiongozi mkubwa wa nchi.


Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "WABUNGE WACHARUKA WATAKA MAKONDA AITWE NA KUHOJIWA"

Back To Top