Mnamo tarehe 17/3/1953 mtaalam wa vyombo vya usafiri wa anga anajulikana David warren mwenye asili ya nchi ya australia aligundua kifaa kitakachoweza kutunza kumbukumbu zote za muhimu ktk safari nzima ya ndege kinachojulikana kama (Black box).
Hamasa hii ilikuja baada ya kutokea ajali ya ndege ya Havilland comet na kubaki bila ya majibu kwanini,ilikuwaje mpaka ikatokea.
Kifaa hiki cha black box kina mifumo ya njia mbili yana (flight data record) (FDR) yani kunukuu kumbukumbu zote za ndege,kama mwenendo wa injini ya ndege,kiwango cha mafuta,hali ya hewa ndani na nje,umbali kutika usawa wa bahari,spidi ya ndege n.k.
Upande wa pili wa kifaa huki unaitwa kama (cockpit voice recorder) (CVR) kikiwa na kazi za kutunza kumbukumbu za sauti za marubani,wasaidizi,abiria,maongezi baina ya marubani na waongoza ndege chini.
Kifaa hiki hukaa au huwekwa ktk mkia wa ndege mwishoni kabisa ili kuepusha kisiharibike pindi ndege itakapopata ajali,huvumilia moto mkali hadi digrii 2000 elfu mbili bila kuungua.
Huvumilia hata muanguko wa nguvu ya elfu tatu na minne(3400 Gs),kinaweza kukaa chini ya maji kufikia futi elfu ishirini 20000 bila kuharibika wala kuingia maji.
Uwezo wa betrii yake inaweza kaukaa na chagi kwa siku 30 bila kuzima na kukaa miaka sita bila seli zake bila kufa.
Kifaa hiki kinajulikana kama black box yani boksi nyeusi lakini kiukweli rangi yake halisi ni rangi ya chungwa(orange).
Black box ina uwezo wa kutunza kumbukumbu zote za ndege kwa zaidi ya Massa 25 ishirini na tano na Mawili kww sauti pekee.
Kifaa hiki ni muhimu sana kwa usafiru wa anga kwani usaidia mambo mengi sana pindi ndege inapopata ajali au kupotea uweza kusaidia kujua nini kilijili kabla ya ajali,kifaa hiki kinaweza kutambukika popote kilipo kwa maili kumi na tano kutoka kilipo kwani kimefungwa mtambo ea GPRS.
Mnamo mwaka 1960 kifaa hiki kilianza kutumika rasmi na mashirika yote ya ndege za abiri na mizigo na kusaidia kujua matatizo mengi yanayotokana na usafiri wa anga.
0 Comments "JE WAJUA KUWA (BLACK BOX) NDIO KIFAA MUHIMU ZAIDI KTK USAFIRI WA ANGA"