
Maandamano hayo yalizaa vita ya wenyewe kwa wenyewe baina ya majeshi ya serikali na makundi ya kabila maarufu la wahauthi wanaotaka kuchukua madaraka ya nchi hiyo,hata hivyo uoinzani ulikua mkali pande zote mbili kiasi kufanya vita hiyo kudumu kwa zaidi ya miaka miwili sasa bila kuisha huku ikiacha maelfu ya watu wakikimbia nhi,kuuwawa,kokusa huduma za msingi kama makazi,elimu,chakula,kushindwa kufanya shughuli za kiuchumi na kufanya mamia kwa maelfu ya watu hasa wanawake na watoto kufa kwa njaa na kukosa maji kabisa.
Kwasasa yemen imekuwa ikatawaliwa na makundi ya kigaidi yenye mafungamano na mtandao wa al-qaeda na kuifanya kuwa nchi ngumu kuishi kwa kukosa nishati ya umeme,usalama wa raia,matukio ya ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia. mashirika ya haki za kibinadamu na kutoa misaada ya kiutu yamethibitisha kuwa sasa yemen iko ktk baa la matatizo hasa ukosefu wa chakula na maji ambayo ni muhimu kwa uhai wa kibinadamu.
0 Comments "VITA,UMASIKINI NA NJAA VYAIMALIZA YEMEN"