
Sababu zilizotajwa kwanini somalia inaongoza kwa ufisadi na rushwa kuwa chanzo kikuu ni vita na umasikini ulikithiri kwa wananchi wa eneo hilo kwa kazi zote za uazlishaji kusimama kabisa,ukosefu wa kazi za kuajiliwa,kukosa amani kwa watu,mauji ya watu kutokana na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
Ikumbukwe miaka ya hivi karibuni makundi mbalimbali ya uharamia wa baharini na kuteka mei za miazigo zilizokuwa zinapita pwani ya somalia na kudai kiwango cha pesa kwa makampuni yanayomiliki meli hizo.
Somalia inatawaliwa na makundi ya kivita na koo mbalimbali kama za al-shabab,mahakama za kiislamu na mababa wa kivita na kufanya somalia isitulie na kuwa na amani ya kudumu hasa ktk mji mkuu wa mogadishu ambapo nui makao makuu ya serikali ya somalia.
Eneo la somalia inalindwa na majeshi ya umoja wa afrika (AMISON) na umoja wa mataifa(UN) kwa miaka kadhaa sasa.
Kwasasa somalia ianasumbuliwa na njaa,ukosefu wa ajira,miundombinu mibovu na michache,huduma duni za afya,elimu duni na idadi kubwa ya watu wanaokimbia nchi hiyo kwenda taifa jirani la kenya na djibout.
Rushwa na ufisadi ndio tatizo kubwa la nchi ya somalia lililosababishwa vita hiyo,hivi karibuni wamefanya uchaguzi mkuu na kumpata Rais Farmajo.

0 Comments "SOMALIA YASHIKA NAMBA MOJA KWA UFISADI DUNIANI"