
Ummi mwalimu aliondeza kuwa ktk tafiti za wizara ya afya zilizofanywa wameona na kugundua kuwa rika la vijana umri wa kuanzia baleghe miaka (15-45) ndio wanaonekana kupata maambukizi zaidi kuliko rika nyingine.
Aliongeza kuwa wasichana wa rika la baleghe (15-19) wanaonekana kuwa na maambukizi ya asilimia 1% zaidi kuliko wavulana ambao wao wana aslimia 0.1%,na wasichana wenye umri wa miaka 20-24 wao wanamaambukizi ya asilimia 4% ukilinganisha na wavulana wao wana 2% kwa rika hiyo.
Waziri aliongeza kuwa baadhi ya makundi ya watu wao wako ktk maambukizi zaidi kuliko wengine ni kama wasichana wanaojiuza(changudoa) wao kila watu 100 basi 26 wanaishi na ukimwi na kila mashoga 100 basi 25 wanaishi na maambukizi hayo na kwa ujumla kila watanzania 100 basi watanzania watano 5 wanaishi na maambukizi hayo.
Ummi aliongeza kuwa wamepiga marufuku baadhi ya Taasisi za kuhudumia na kutoa elimu za afya na ukimwi zimegundulika kuhamasisha zaidi matendo kama ya ndoa jinsia moja,ushoga na usagaji hivyo wamezipiga marufuku na kusema kuwa huduma zote zitatolewa na vituo,hospitali na zahanati za serikali.
0 Comments "MAAMBUKIZI YA UKIMWI KWA WASICHANA YAKO JUU KULIKO WAVULANA"