HOSPITALI YA MILEMBE YAFURIKA WAGONJWA

Hospitali kubwa ya wagonjwa wa akili maarufu kama Milembe iliyopo mjini dodoma makao makuu ya nchi.

Wataalam wa afya wa hospitali hiyo ya milembe wamezungumza kuwa idadi ya wagonjwa wa akili inazidi kuongezeka zaidi hasa kwa miaka ya hivi karibuni kiasi cha kushindwa  kuhudumia kwa ufanisi kutoka na eneo la kuwaweka na vifaa vya kuwahudumia kutkana na idadi ndogo ya wahudumu ikiwemo madaktari na wauguzi.

Tathimini iliyofanywa juu ya kuonekana na kuongezeka kwa wagonjwa wa akili ktk hospitali ya milembe na nchini kwa ujumla ni swala zima la kuongezeka kwa matumizi ya madawa ya kulevya na unywaji wa pombe,watu wengi hasa rika la vijana zaidi ndio lianaongoza ktk matumizi ya bange,milungi,kokeni.heloini,madraksi.

Matumizi makubwa ya aina hii ya madawa inapelekea watu wengi kupata magonjwa ya akili kwa kasi kubwa,hivyo juhudi za kupiga vita usambazaji,uuzaji na utumiaji wa madawa haya ni wa muhimu sana ili kulinda afya ya akili za wananchi wetu.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "HOSPITALI YA MILEMBE YAFURIKA WAGONJWA"

Back To Top