
Watu umimika kutoka miji mingi duniani kuja kuona na kurahia maisha kwa ujumla kwa zaidi ya wiki mbili mfululizo usiku na mchana watu ufurika mitaani kwa kupita wakcheza,kuimba na kuvaa mapambo ya nguo,vinyago ya aina mbalimbali ya kutisha na kuchekesha watu.
Sherehe hizi zinaheshimika sana na watu wa huko na wanaamini ni ktk kulinda utamaduni wa wazee wao waliokuwepo kabla yao,lakini pia uongeza mapato serikalini,manunuzi ya mavazi,vinyago na vyakula na kukodi kwa hoteli ktk mji mkogwe barani ulaya ambao utembelewa na watalii wengi kutoka sehemu nyingi za uleimwengu.
Venice (venezia) ni mji uliopo ktk maji kabisa na uzungukwa na majengo yalianzia ktk maji na watu wake utumia usafiri wa boti na ngalawa ndogo ktk shughuli za kila siku na kwenda eneo olote lile ndani ya mji huo.
Sherehe kama hizi pia ufanyika maeneo mengine ya dunia kama Brazil ktk miji ya sao paulo,rio de jeneiro,brasilia watu huvaa nguo za kungara na mapambo ya aina nyingi kiasi kwamba hutoweza kumtambua mtu kwa uraisi hata kama ni ndugu yako,mbwembwe nyingi uendelea kwa mda wa wiki mbili mfululizo.
0 Comments "SHEREHE YA KUVAA VINYAGO ZAENDELEA ITALIA"