JE WAJUA KUWA KUKAA SANA NDANI NA KUTUMIA MWANGA USIO WA ASILI KWA MUDA MREFU UPUNGUZA UWEZO WA MACHO KUONA

Wataalam wa mambo ya afya wanasema watu wengi upoteza uwezo wa macho yao kuona hasa kwa nchi zilizoendelea kwa sababu ya kukaa sana ndani na na kutumia vifaa vya umeme vyenye kutoa mwanga usio asili kwa mda mrefu.

Kwa mataifa ya marekani na ulaya watu wengi wanaumia kukaa sana ndani ya majengo kwa mda mrefu ktk maisha yao ya kila siku na kulazimu kutumia mwanga wa taa za vifaa kama simu,kompyuta ktk shughuli zao za kila siku,hivyo kufanya kutokuwepo nnje na kupigwa na mwanga wa jua ambao ni muhimu ktk kuongeza wa kuona kwa mtu.

Wataalam wanasema kuwa mwanga wa jua na wa asili unasaidia sana ktk kufanya macho ya mtu kuendelea kuona vyema,hivyo swala la mtu kukaa ndani kwa mda mwingi bila kukutana na mwanga wa asiliwa jua anaweza kupoteza uwezo wake wa kuona mapema kabisa akiwa bado mdogo sana.

Ugonjwa huu wa macho unajulikana kama (myopia) macho ya mtu huwa hayana uwezo wa kuona mbali zaidi ya vitu vya karibu tu,hii hutokana aina ya watu ambao wanatumia mda mwingi kukaa ndani na kutumia mwanga hafifu na si wa asili ambao ufikia mahali uharibu na kupunguza uwezo wa macho yao kuoa mbali tena. watu ambao wako ktk hatari ya kupatwa na ugonjwa huu ni baina ya umri wa miaka (12-50).

Wataalam wanashauri kwa watu wajitahidi sana kutumia mwanga wa asili ambao unatokana na jua pia kupunguza matumizi ya vifaa vinavyotoa mwanga usio wa asili (artificial)kwa mda mrefu kama simu,kompyuta n.k.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "JE WAJUA KUWA KUKAA SANA NDANI NA KUTUMIA MWANGA USIO WA ASILI KWA MUDA MREFU UPUNGUZA UWEZO WA MACHO KUONA"

Back To Top