SAUDI ARABIA YAISHUTUMU VIKALI IRAN KWA KUSAIDIA UGAIDI DUNIANI

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa bwana Adel bin ahmed al jubeir wa Saudi Arabia ameipiga jiwe iran kwa kusema iran ndio inch inayoongoza kwa kuvipa nguvu vikundi vya kigaidi ili viweze kutekeleza matukio hayo sehemu mbalimbali duniani.
Akihojiwa na kituo cha runinga cha habari cha TRT WORLD waziri huyo ameituhumu iran kwa kuwapa nguvu ya pesa,silaha na mikakati makundi mabalimbali ya kigaidi la  Hizbullah la  Lebanon,shia la  Iraq,Taliban nchini Afghanistan,vikundi vya syria na kufanya mashariki ya kati kutokuwa na amani ya kudumu.

Iran hivi karibuni ilifanya majaribio ya maombola yake ya masafa ya mbali (long range missile) na kukosolewa na mataifa ya ulaya ikiwemo na marekani na kulazimisha rais wa marekani Donald trump kuongeza vikwazo vipya vya kiuchumi juu ya iran.

Hii si Mara ya kwanza kwa Iran kujaribu silaha hizo na kusema inatengeneza silaha hizo kwa ajili ya kujilinda iwapo itavamiwa au kutishiwa usalama wake.

Tayari iran kwa miaka kadhaa inashutumiwa kwa kutengeneza silaha za kinyuklia na kukana jambo hilo  na kusema nyuklia ni  kwa ajili ya kuzalisha umeme tu na si  vyenginevyo.
Toka mapinduzi ya kiislamu kufanyika mwaka 1979 Iran imekuwa nchi isiyoaminika na maswala  ya usalama na mataifa mbalimbali,kwasasa iran inaongozwa na Rais  Hassan rohan.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "SAUDI ARABIA YAISHUTUMU VIKALI IRAN KWA KUSAIDIA UGAIDI DUNIANI"

Back To Top