MBOWE AVUNJA UKIMYA KUHUSU MADAWA YA KULEVYA

Mwenyekiti taifa wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Mh. Freeman mbowe amavunja ukimya kwa kuongea Jana na vyombo vya habari juu ya shutma ya kujihusisha na madawa ya kulevya.

Mwanzoni mwa wiki hii Mkuu wa mkoa wa dar es salaam Mh.Paul makonda alitaja orodha ya watu wanaohusika kwa njia moja au nyingine ktk sakata la  madawa ya kulevya nchini hasa mkoani Dar es salaam.
Orodha hiyo ilitaja watu zaidi ya 65 akiwemo Yusuph manji,idd azan,askofu gwajima akiwemo na mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo bwana Freeman mbowe kuwa anahusika na kashfa hiyo.
Licha kuambiwa ifikapo ijumaa waripoti kituo kikuu cha polisi baadhi ya yao walifanya hivyo kwa Siku ya alhamisi na ijumaa lakini mbowe hakufanya hivyo.
Jana akiongea na vyombo vya habari mbowe alikili kuwa wito ameusikia na anaunga mkono swala kupambana na madawa ya kulevya kwa asilimia mia moja lakini hakuitikia wito kwa sababu ya aliemwita hausiki na na hana mamlaka ya kufanya hivyo kwani viko vyombo maalum vinavyohusika na kazi hiyo,pili njia zinazotumiwa ktk kushughulikia jambo sio sahihi na zinakiuka haki za kiutu ukizingatia watu wana vyeo na nyadhifa za juu,wana familia.

Aliongeza kuwa serikali imechelewa kulifuatilia jambo hili  kwani limeshaota mizizi na watu wanaofanya biashara hizo wengi  no kutoka chama tawala(ccm) hivyo wanabebana.
Njia ya kuita watuhumiwa hadharani kwenye vyombo vya habari sio sahihi kwani unafanya wahusika kuficha ushahidi wote  kabla hujaenda kuwapekuwa hivyo njia hiyo inapoteza kabisa uhalisia wa makosa ya jinai.
Mbowe alisema atatii agizo lolote kutoka kwenye mamlaka inayohusika na mambo ya madawa ya kulevya na sio kuitwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MBOWE AVUNJA UKIMYA KUHUSU MADAWA YA KULEVYA"

Back To Top