MKULIMA AFIKISHWA KIZIMBANI KWA KUSAIDIA WAHAMIAJI HARAMU KUINGIA UFARANSA

Mkulima mmoja bwana Cedric herrou wa huko nchini ufaransa amefikishwa mahakamani baada ya kukutwa na kosa la  kusaidia wahamiaji haramu kuingia inchini humo na kupigwa faini ya dola 32000 sawa na milioni sita na laki nne  za kitanzania (640000).
Mkulima huyo ambae alikuwa anawapitisha wahamiaji hao kupitia shambani kwake wakiyokea nchi ya Italia na kuwasadia kwa usafiri,chakula na mambo mengine.
Mkulima huyo alijitetea kuwa watu wana shida na matatizo mengi haswa kutoka nchi za kiafrika na Asia kwa kukimbia njaa,vita na maisha duni yaliopo ktk nchi zao na kukimbilia nchi za ulaya na marekani ili wapate kazi na maisha yenye nafuu.
Alisema kuwa yeye kamwe hatoacha kusaidia wakimbizi na anapinga kabisa Sera za ulaya na marekani za kuzuia wakimbizi na wahamiaji kuyoka mataifa mbalimbali kwani ni  kukiuka haki za kibinadamu.

Kwa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la wahamiaji kutoka mataifa ya afrika magharibi,kaskazini,Iraq,Syria wakiwa wanakimbia vita na machafuko ktk nchi zao kukimbilia ncha ujerumani,Italia na ulaya mashariki.
Rais  Donald trump amepiga marufuku mataifa saba kuingia marekani zikiwemo Iran,Syria,Iraq,afghanstan kwa kusema wanaleta vitendo vya kigaidi nchini.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MKULIMA AFIKISHWA KIZIMBANI KWA KUSAIDIA WAHAMIAJI HARAMU KUINGIA UFARANSA"

Back To Top