RAIS MAGUFULI AMUAPISHA MKUU WA MAJESHI MPYA

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.john pombe Joseph magufuli amemuapisha Mkuu wa majeshi mpya leo ikulu mapema.

Mkuu huyo  wa majeshi anaejulikana kama Venance S.mabeyo alietuliwa wiki iliyopita ktk sherehe za wiki ya mahakama ambapo mgeni rasmi alikua raisi  magufuli.

Pia raisi  magufuli amemuapisha Mkuu na mnadhimu wa chuo cha ulinzi cha jeshi ndugu aloyce mwakibolwa.
Nafasi ya Mkuu wa majeshi iliachwa wazi na Mkuu wa zamani Davis mwamunyange.

Dk magufuli amezungumzia sakata swala la  madawa ya kulevya linalotokota wiki hizi,kuwa kashfa hizo hazina umaarufu wa ukubwa,vyeo au ukaribu wa mtu  yeyote ataketuhumiwa akamatwe na sheria ifuate mkondo wake hata kama atakuwa mke  wake(Janeth) akamatwe tu.

Aidha alimwambia IGP Ernest mangu kuwa anajua alipigiwa simu na watu kuwa apunguze nguvu kutaja wahalifu Ila hakuwasikiliza kabisa na endapo angefanya huvyo basi leo cheo kile asingekuwa nacho tena.

Mkuu wa mkoa Dar es salaam amepongezwa kwa bidiii na jitihada anazozionyesha juu ya swala hilo,lakini pia ameongeza kuwa hakufanya uteuzi wa Mkuu mpya wa majeshi kwa kuhofia kuona watu wangehisi amemtumbua Davis mwamunyange.

Sherehe hizo zimehudhuriwa na raisi wa Zanzibar dk Mohamed shein,waziri mkuu majaliwa kassim majaliwa.


Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "RAIS MAGUFULI AMUAPISHA MKUU WA MAJESHI MPYA"

Back To Top