PAUL MAKONDA ATEMA CHECHE ZAIDI DAR

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bwana Paul makonda ametema chehe leo hii 13/2/2017 ktk mkutano akiwa ameambatana na kamishna wa polisi mkuu mkoa Simon sillo,kamishna rogers william siyanga na baadhi ya watu wanaotumia madawa hayo kama msanii Tid wa mziki wa kizazi kipya na kutoa ushuhuda wake kuwa kweli madawa ya kulevya yaliaathiri sana maisha yake na hata mahusiano  na jamii kiujumla.

Paul makonda amezidi kukazia kuwa anayo orodha mpya ya watu tisini na saba (97) wanaohusika na utumiaji,uuzaji na uingizaji wa madawa ya kulevya,ameongeza kwa kusema yeye ataendelea na nguvu zaidi ktk  jambo hilo kwani ni kubwa na ni hatari sana  kwa uhai na maendeleo ya kizazi cha taifa hili.

Makonda alliongeza wako watanzania wanachukua pasipoti zaidi ya moja ili kufanikisha shughuli hiyo,zipo hoteli na kumbi za starehe  nyingi jijini dar es salaam zinahusika na uuzajin wa madawa ya kulevya,aidha alisema miongoni mwa njia mpya wanazotumia ni kuwka dawa za kulevya ktk mitungi ya gesi na kuingiza nchini.

Idadi ya watanzania waliokamatwa na kufungwa nchi ya afrika kusini pekee ni zaidi (297) ukiachana na nchi nyingine duniani kama china,uganda,dubai n.k.

Wachangiaji wengine waliongeza kwa kusema kuwa kwa watumiaji wa milungi pekee wako kwenye hatari ya kupata kansa ya mdomo,koo na tumbo na kufanya mwanamme kukosa nguvu za kiume na kauharibu ndoa.


Orodha ya madawa ya kulevya itakuwa kwa awamu saba ili kufikia mwisho na wataanza toka kipindi cha utawala wa awamu  ya pili hadi huu wa tano.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "PAUL MAKONDA ATEMA CHECHE ZAIDI DAR"

Back To Top