JPM APIGILIA MSUMARI KUHUSU MADAWA YA KULEVYA

Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania John pombe joseph magufuli jana akiwa ktk mkutano wa kuapisha kamishina wa madawa wa kulevya Bwana rogers william siyanga,kamishina uhamiaji anna peter makakala,balozi nchini ubeligiji bwana edward sokoine,balozi wa algeria omar yusuph mzee,balozi wa uganda grace aron mgovano aliowateua hivi karibuni.

Mh.magufuli alionelea jambo la madawa ya kulevya ambalo kwa sasa linafuka moshi na kufanya baadhi ya watumiai,wasambaji na wamiliki wa biashara hizo kuitwa kituo kikuu cha pilisi na kuhojiwa wengine kuruhusiwa na wengine kushikiliwa hadi sasa,baadhi ya watu hao ni mfanyabiashara yusuph manji,mchungaji gwajima,idd azan.

Rais magufuli alipigilia msumali kwa kusema vita hii ni kali na anaiunga kwa nguvu zote na atahakikisha kuwa anaipa nguvu kubwa vita hiyo na kusema watu wote wanaohusika na biashara hiyo watakamatwa na kushughulikia,aliongeza kwa kusema kuwa watanzania wote ambao wamekamatwa nchi za nnje kwa makosa ya madawa ya kulevya na kufungwa huko basi hatahusika kwa njia na msaada wowote ule ktk kusaidi wao kutoka,bali ameagiza vyombpo vyote vuachane na watu wa aina hiyo kama watafungwa au kunyongwa basi hiyo itakuwa ni juu yao ila sio kuhusisha mabalozi ktk mambo hayo.

Pia alizungumza na kamishina wa polisi simon sillo kuwa tukio la wanakwaya wa askofu gwajima kuja kituoni na kuimba nyimbo na swala watu kudeki barabara kwa ujio wa manji kituoni,amechukizwa na tabia hiyo na kuagiza kuwa watu wasizoee vituo vya polisi wa mtindo huo na kama watarudia basi wachukuliwe hatua za kisheria.

Anahitaji vituo vya polisi kuheshimiwa kama wanavyiheshimiwa jeshi la wanachi (JWTZ).

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "JPM APIGILIA MSUMARI KUHUSU MADAWA YA KULEVYA"

Back To Top