NOKIA 3310 (JENEZA) KURUDI SOKONI UPYA MWEZI HUU

Kampuni kubwa na iliyowahi kutamba sana kwa kutengeneza simu imarangumu na rahisi kutumia duniani kote ya (NOKIA) imekusudia kutengeneza na kurudisha sokoni upyasimu ya nokia 3310 al maarufu kama nokia jeneza kama watanzania walivyozoea kuziita baada ya maoni ya wateja na maombi mengi kutoka pande  zote za dunia.

Sababu ya kampuni na wateja kutaka simu hii kurudi sokoni upya inatokana na uimara wake wa kipekee,kutunza chagi kwa mda mrefu,hata ikianguka huwezi kuvunja kioo wa kasha lake zaidi ya kutawanyika kisha ukivifunga pamoja simu itafanya kazi kama kawaida bila tatizo lolote.

Simu hii iliyozinduliwa kwa mara kwanza sokoni tarehe 1/9/2000 na kuuza zaidi ya simu miliomi 126 duniani kote ni zaidi ya miaka 17 sasa toka kuanza kutumika kwa mara kwanza kampuni hii inasifika kwa kutengeneza simu imara kutoka ktk viwanda vyake vya ulaya hungary na makao makuu nchini finland.

Mauzo ya simu za nokia yalishuka baada ya makampuni mengi kutoka china kuanza kutengeneza kwa wingi na bei nafuu,kampuni kama(huawei,techno,itel,ditel,zte na kuua kwa kiasi kikwabwa cha mauzo ya simu za nokia,motorola,siemens,alcatel.sony ericson,sony,panasonic n.k.

Simu ya nokia 3310 inatarajiwa kurudi sokoni mwishoni mwa mwezi huu,kuna msemo usemao kuwa huwezi kuvunja nakia 3310 kwa baadhi ya vitu ila unaweza kuvunja baadhi ya vitu kwa kutumia simu hii na yenyewe ikabaki salama,kwa wale waliowahi kutumia simu hizi za nokia wanajua vizuri uimara wa simu kutoka kampuni hii ya nokia.

Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme

Related Post:

0 Comments "NOKIA 3310 (JENEZA) KURUDI SOKONI UPYA MWEZI HUU"

Back To Top