NJAA IMEKUWA TATIZO SUGU BARANI AFRIKA NA MASHARIKI YA KATI

Shirika la chakula duniani WFP (world food program) na lile la AMNESTY INTERNATIONAL ambayo yote yako chini ya umoja wa mataifa (UNITED NATIONS)  yamesema kuwa njaa ktk mataifa ya Nigeria,sudani kusini,somalia,yemen,syria limaekuwa ni janga la kimataifa kwani sehemu kubwa ya wananchi wanataabika kwa njaa kali hasa watoto na kina mama.

Maeneo yote haya yamekuwa yana hali hiyo ya njaa ikiwa ni tatizo la kutengenezwa na binadamu wenyewe na wala siyo la kiasili,sehemu hizi zote zimekuwa na vita za wenyewe kwa wenyewe kwa muda mrefu ktk kugombea madaraka baina ya waasi na serikalimlakini pia sababu nyingine ilitajwa kuwa ni mabadiliko ya hali ya hewa ktk dunia inafanya kukosekana  kupatikana kwa mvua za kutosha na kusababisha ardhi kuwa kame.

Jamii kubwa ya watoto wamekuwa wakiugua magonjwa ya utapiamlo na  wengi wanakufa kwa kukosa chakula kabisa,nchi ya naigeria kaskazini kumekuwa na mapambano na kundi la boko haram ambalo linasumbua maeneo hayo kwa muda mrefu,somalia kumekuwa na mapigamo ya koo toka mwaka 1991,yemeni kugombea madaraka.

Hali hii ya kupoteza uhai wa watu wengi kwa kuendekeza maslahi binafsi ya kutaka madaraka imekewa vikali na wala haikubaliki na umoja wa mataifa (UN) kwani inazoletesha maendeleo na kufanya watu kushindwa kufanya shughuli za uzalishaji mali.





Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme

Related Post:

0 Comments "NJAA IMEKUWA TATIZO SUGU BARANI AFRIKA NA MASHARIKI YA KATI"

Back To Top