
Manji alianza kwa masikitiko makubwa na kusema alichokifanya mkuu wa mkoa wa dar es salaam ni kumchafulia jina lake kubwa duniani hasa ukizingatia yeye ni mfanya biashara mkubwa ndani na nje ya nchi,lakini pia yeye ni mwenyekiti wa timu ya yanga na anayo heshima kubwa hivyo swala swala la yeye kuhusishwa na kashfa hiyo ni sawa na kuichafua klabu ya yanga ambayo inafahamika afrika nzima,aliongeza kuwa kama mkuu wa mkoa anataka kusaidiwa kutaja watu wanaohusika na madawa ya kulevya basi angemwita kisirisiri na sio kumuanika hadharani kama ilivyofanyika.
Yeye manji anakusudia kwenda kuripoti kesho kitupo cha polisi na sio ijumaa kama ilivyotakiwa kwani hataki kupanga foleni kubwa ya watu 65 itakuwa inamaliza mda wake wa kutekeleza majukumu mengine ya biashara zake,kwani hivi karibuni anatarajia kwenda nchini comoro.
0 Comments "MUDA MCHACHE BAADA KUTAJWA MANJI KTK ORODHA YA WATUHUMIWA WA MADAWA YA KULEVYA AONGEA NA VYOMBO VYA HABARI"