MPINZANI MKUU WA SERIKALI YA CONGO DRC AFARIKI

Kiongozi wa kambi ya upinzani bwana Etienne tshiseked amefariki dunia akiwa ktk matibabu huko brussels nchini ubeligiji,kifo cha kiongozi huyo wa chama cha UDPS kimezua taharuki na mshangao mkubwa kwa wakongo na wanachama wote kwa ujumla kwani amekufa akiwa karibuni na uchaguzi mkuu ambao mwaka huu umezua mgogoro mkubwa na kuamuru kwa raisi joseph kabila kuachia nafasi ili kupisha uchaguzi wa raisi mpya.
Etienne amafariki akiwa na umri wa miaka 84,pia elishawahi kushika nyadhifa ya uwaziri wakati wa utawala wa dikteta mobutu sese seko alietwala kuanzia mwaka 1965-1997 kisha kufuatiwa na kiongozi mwingine bwana Laurent kabila ambae alikufa baada ya kupigwa risasi na mlinzi wake.
Taifa congo drc au zamani lilijukana kam zaire ni taifa linaloongozwa na machafukomya kugombania madaraka kwa miaka mingi na kufanya kuwa miongoni mwa mataifa masikini sana duniani licha ya kuwa na rasiluimali nyingi za mdini ya dhahabu,shaba,almasi,mekyuri,kuwapo na misitu mikubwa  na meeneo makubwa ya ardhi yenye rutuba yanayofaa kwa kilimo.
Congo imekuwa na maeneo korofi kama jimbo la kivu kaskazini na kusini,katanga amabapo vikosi vya waasi vimejificha misituni na kufanya mauaji,ubakaji,uchimbaji wa madini,kutumikisha watoto ktk jeshi.
Mji mkuu wa congo unafahamika kama kinshasha.
Kifo cha etienne kimeleta pengo kubwa ktk siasa za kuleta mapinduzi na demokrasia ya kweli kwa taifa hilo la ya kati ambalo ina eneo kubwa.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MPINZANI MKUU WA SERIKALI YA CONGO DRC AFARIKI"

Back To Top