MOTO WA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA WAANZA KUTEMA CHECHE UPYA

Mkuu wa mkoa wa dar es salaam mh. Paul makonda ametema Chechen zake kwa Mara ya pili Leo kwa kuwaambia watu wanaohusika na kuingiza,kusambaza,kuuza na hata wale wanaotumia madawa ya kulevya amejitoa sadaka kupambana juu ya janga hilo kubwa kitaifa na hata kidunia ambalo linamaliza nguvu kazi vijana.
Makonda amekamata baadhi ya watu wakiwa na dawa za kulevya na tayari ameshajipanga kuhakikisha wale wote wanaohusika na michezo hiyo wanatiwa mbaloni na kushtakiwa.
Baadhi ya watu maarufu na wasanii kama wema isack sepetu,tid,child Benz,recho wamehusishwa na mitandao hiyo ya madawa na kuamliwa kesho kufika kituo cha polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Itakumbukwa Paul makonda sio kiongozi wa kwanza kujaribu kukemea mambo ya madawa ya kelevya,huko mwanzo Marehemu mbunge wa kuteuliwa ccm vijana aliwahi kugusia jambo hili,waziri wa usafirishaji na uchukuzi Harison mwakyembe kupitia njia za uwanja wa ndege pia alitaka mashine kufanya kazi ya kuchunguza mizigo ili kuzia uingizaji wa madawa.
Madawa ya kuelevya ni  hatari sana kwa uchumi,Afya na hata kwa maendeleo ya mtu  mmoja mmoja na hatimae kwa taifa kiujumla,kiasi kikubwa cha watumiaji wa madawa haya ni  vijana kuanzi miaka ishirini (20) na kuendelea ambao ndio nguvu kazi.
Maisha,ndoa na hata familia nyingi zimesambaratika kutokana na matumizi ya madawa,madawa ya kulevya ni  biashara ya watu wa kati na juu! Wasanii na wanamichezo Wengi wanahofiwa kuathirika na matumizi ya madawa kama child Benz,ray c na wengine kupoteza maisha kabisa.
Kifupi madawa ya kulevya yana madhara mengi sana kwa jamii licha ya faida kubwa wanayoipata wafanyabiashara wenyewe.


Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MOTO WA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA WAANZA KUTEMA CHECHE UPYA "

Back To Top