MIAKA SITA YA WALIBYA BILA KANALI MUAMMAR GADDAFI

Walibya leo wanasheherekea miaka sita toka kuanguka kwa utawala wa kiongozi huo alioonekana shupavu barani afrika na hata machoni mwa mataifa ya ulaya.

Muammar mohammed abu minyar gadadafi (kanali muammar gaddafi) ni mwanapinduzi aliezaliwa 7/6/1942  huko qasri abu hadi libya na kuuawa huko sirte 20/10/2011akiwa na umri wa miaka 69 na waasi walikuwa wanapigania nchi hiyo.

Gaddai lioa mke wa kwanza fatiha al nur 1969-1970 na mke mwingine ajulikane kama safia farkash 1970-2011 alipouawa,gaddafi alibahatika kupata watoto kam seif al islam,ayesha n.k
Gaddafi alishika cheo cha uwaziri mkuu mwaka 1970-1972 na kufanya mapinduzi 1979 na kuitawala nchi hiyo kwa mkono wa cvhuma hadi alipouawa mwaka 2011.

Elimu ya gaddafi iliigamia zaidi ktk mambo ya kijeshi na alisoma vyuo vya sertvice command and staff,benghazi military university,university of libya,mpaka anakufa gaddafi alishaandinka vitabu kama The green book,escape to hell,my vision,

Muammar gaddafi alijulikana zaidi kwa ushupavu wake hasa kwa mataifa ya magharibi yaliojaribu kuingilia mambo ya ndani ya nchi yake au afrika,alikuwa adui wa marekani na hata mataifa mengi ya ulaya ikiwemo uingereza kwa utuhumiwa kutuma na kufadhili vukundi vya ugaidi duniani vinavyofanya uhalifu kama ndege iliyoanguka uingereza  kwa kulipuliwa.

Gaddafi pia laisifika kwa kuasaidia mataifa mengi ya afrika kijeshi na hata kiuchumi,pia laiijenga sana nchiya libya hasa mji mku tripoli,benghazi kwa kutumia uchumi na pesa nyingi zilizopatiaka na uchimbaji na uuzaji wa mafuta duniani. alijenga vyuo,hospitali,shule na kutoa elimu bure kuanzia awali hadi chuo,huduma za kijamii kama maji na umeme vilikuwa bei sawa nba bure,watu kulipwa kabla ya kuanza kazi,kupewa pesa yam kuolea.

Gaddafi alitetea sanma wazo la afrika kuungana na kuwa taifa moja lenye serikali moja tu ili kuleta umoja na nguvu kwa bara afrika.

Mwamko wa watu bara arabu kuhitaji utawala wa demokrasia zisha ndio ulianzisha vuguvugu hilo kwa nchi za tunisia,yemen,misri na hata libya.

Kwasasa toka kifo cha gadaffi 2011 maisha ya libya yamekuwa magumu na wanachi wanalalamika hali hiyo kwa kusema hawaoni mabadiliko yeyote ya msingi toka kuabaki wakiwa na serikali mpya,mfumuko wa bei,wakimbizi,vita za wenyewe.

Muammar gaddafi aliapa kufia nchini kwake na asingekimbia popote ila kufia ktk ardhi ya libya na ndivyo ilivyokuwa alipokamatwa na kikundi cha wanajeshi na kupigwa na mawe kisha kubuluzwa barabarani na gari.





Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme

Related Post:

0 Comments "MIAKA SITA YA WALIBYA BILA KANALI MUAMMAR GADDAFI"

Back To Top