MIAKA 30 JELA KWA WAZAZI AU MTU ATAKAYEMPA MIMBA MWANAFUNZI

Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa akiwa ktk ziara yake  mkoani manyara ktk wilya za babati,kiteto na mbulu amewahutubia wanachi maeneo mbalimbali na kusisitiza swala la elimu kwa watoto hasa wasichana ambao wanaonekana kuwa na changamoto nyingi ktk kufikia malengo yao.

Kauli hii imekuja baada ya kuwepo kwa malalamiko mbalimbali uya changamoto ya elimu ikiwemo swala la umbali kutoka nyumbani na shule zilipo,ukosefu wa miunndombinu ya msingi inayotosheleza,walimu wasiotosheleza na ukosefu wa vifaa vya maabara na jambo la watoto wa kike wengi kushindwa kufikia tamati ya elimu yao kutokana na kupewa ujauzito wakiwa masomoni na kushindwa kufgika lengo la kumaliza shule.

Waziri mkuu Majaliwa ikamlazimu kutoa kauli kali na nzito kwenda kwa wazizi kuwa endapo mtoto wa kike atapata ujauzito au kuolewa basi wazazi hao watachukuliwa hatua za kisheria kali ikiwemo kufungwa miaka thelethini jela,pia kwa mtu aliyetia mimba nae atafungwa kwa miaka hiyo.

Wazazi wengi wamekuwa wakifumbia macho vitendo hivi vya watoto wao kuwekwa mimba na wao wakanyamaza au kumaliza kinyumbani,lakini wamekuwa wakiwaozesha watoto na kuwakatiza masomo kwa ajili ya ndoa za utotoni.

Serikali imeajili zaidi ya walimu zaidi ya elfu nne nchini na imekuwa ikilipa gharama zote za masomo hivyo serikali haitokuwa na mchezo kwa  kwa watu watakaochezea elimu .


Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MIAKA 30 JELA KWA WAZAZI AU MTU ATAKAYEMPA MIMBA MWANAFUNZI"

Back To Top