MBOWE AWASHITAKI VIGOGO WA SERIKALI

Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia  na maendeleo (CHADEMA) amefungua kesi mahakama kuu ya tanzania kwa kile kinachosemekana ni juu ya ukiukwaji wa haki za kibinadamu wakati wa kushughulikia swala zima la madawa ya kulevya.

Ikumbukwe kuwa mwanzoni mwa mwezi februari Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh.Paul Makonda aliwataja watuhumiwa wa madawa ya kulevya hadharani ktk vyombo vya habari na kusisitiza walipoti kituo cha polisi,baadhin ya watuhumiwa hao ni kama Wema sepetu,chid benz,Tid,yusuph manji na wengine wengi.

Lakini ilipofika orodha ya pili ambayo nayo pia ilitajwa hadharani ilimtaja mwenyekiti huyo bw. Freemn mbowe kuwa nae anahusika ktk shughuli za madawa na yeye kukataa kufika polisi kwakua alisema mkuu wa mkoa hana mamlaka ya kumwita yeye polisi bali ni RPC Simon sillo.

Kesi hii inakwenda kusikilizwa na ma jaji Sekiety kihiyo,lugano mwandambo na jaji pelagia,mbowe atawashitaki Mh.Paul makonda,kamanda wa polisi mkoa wa Dar es salaam Simon sirro ktk kupinga uataratibu ulitumika ktk kuwashughulikia watuhumiwa wa madawa ya kulevya kwa kuwataja hadharani.

Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme

Related Post:

0 Comments "MBOWE AWASHITAKI VIGOGO WA SERIKALI"

Back To Top