MATEKA WA KIJERUMANI ACHINJWA UFILIPINO

Kundi la waasi la Abu sayyaf la nchini ufilipino limefanya mauaji ya kutisha kwa kumchinja mateka wa kijerumani waliokuwa wanamshikilia toka mwaka jana baada ya kutoa amri ya kulipwa zaidi ya dola laki sita za kimarekani kwa serikali ya ujerumani na wakashindwa kutimiza sharti hilo kwa muda wote.

Mateka huyo Jurgen Gustav kantner mwenye umri wa miaka 70 alietekwa akiwa na mkewe nchini humo na mkewe huyo aliuwawa toka mwaka jana.

Rais wa ufilipino Rodrigo Duterte ameomba msamaha kwa kushindwa kuokoa maisha ya mateka huyo,wakati huo huo kansela wa ujerumani bibi Angela markel amehuzunishwa na kitendo hiko cha kuuwawa kwa mateka huyo kwa kuchinjwa.

Kundi hili la waasi limekuwa likisumbua kwa mda mrefu serikali ya ufilipino kwa mda mrefu na kufanya mauaji mengi ya raia wasio na hatia.


Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme

Related Post:

0 Comments "MATEKA WA KIJERUMANI ACHINJWA UFILIPINO"

Back To Top