MASHABIKI WA YANGA WAONYWA

Mashabiki wa mpira wa miguu wa timu ya yanga afrika wameonywa vikali  juu ya kujiandaa kuvaa mabango au kufanya vitendo vitakavyokuwa na lengo la kukashifu viongozi wa shirikisho la mpira au serikali.

Hii inatokana na mwenyekiti na wa timu hiyo ya soka nchini Yusuph Manji kushikiliwa na polisi kwa zaidi ya wiki moja na kuachiwa jana kwa makosa ya kutumia madawa ya kulevya aina ya heloini na kusimamishwa kizimbana lakini alikana kosa hilo na kuambiwa kulipa dhamana ya pesa taslim ya shilingi milioni kumi nan kuachiwa huru hadi hapo atakapoitwa tena mahakamani.

Viongozi wa shirikisho la mpira wa miguu wamekemea vikali juu ya mambo hayo yaliopangwa na mashabiki na kusema vitendo vya aina hiyo ni vya kihuni na havifai ktk mpira wa miguu na michezo kwa ujumla kwani vinavunja moyo hata viongoz wakubwa wa serikali kama Rais Magufuili alivyosema yuko tayari kwenda kuangalia ndondo cup kuliko kuingia ktk mechi kubwa zisizo na utulivu na kuhgaribu miundombinu iliyojengwa.

Mashabiki hao walikuwa wanataka kufikisha ujumbe kwa serikali na wa mpira wa miguu juu ya kukamatwa kwa mwenyekiti wao wa timu ya yanga na waio kubaki kimya kwa mda wote.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MASHABIKI WA YANGA WAONYWA"

Back To Top