MARUFUKU YA POMBE YA BEI CHEE YA VIROBA YAWAWEKA REHANI WATUMIAJI

Sekeseke la kufuatilia wamiliki,wauzaji,waingizaji,wasambazaji na watumiaji wa madawa hatari ya kulevya limeenda sambamba kabisa na kupiga marufuku kwa pombe halali ya bei nafuu  ya konyagi,zed na tyson
maarufu kama pombe ya VIROBA imeleta sintofahamu kwa watumiaji wa bidhaa hiyo iliyokuwa adimu kwa sasa ktk miji mikubwa hapa nchini na kufanya watumiaji na wamiliki wa biashara hiyo kuwa ktk wakati mgumu ktk biashara hiyo.
Wamiliki,wafanyabiashara na mawakala wakubwa  wa biashara hiyo wametoa malalamiko kwa wazir January makamba kuwa mda waliopewa kwa kuachana na biashara hiyo tarehe 1/3/2017 ni mdogo na utawaletea hasara kubw kwani malighafi na bidhaa hiyo bado iko nyingi kiwandani na sokoni.

Hata hivyo waziri huyo alisema kuwa mda huo unatosha sana tena wamechelewa kwaniahadi ilikua mwezi januari ndio iwe mwisho wa matumizi ya pombe hizo na mifuko laini isiyokidhi viwango husika.

Aidha waziri January aliongeza kuwa athari zinazotokana na matumizmya vilevi hivyo vya bei nafuu nimkubwa sana kulinganisha na faida yake,moja ya matatizo ya pombe hizo ni kwa ajali nyingi za barabarani kwa bodaboda na magari zaidi ya asilimia 68% zinasababishwa na matumizi ya pombe hizo za vioba zinazopatikana kwa bei nafuu.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MARUFUKU YA POMBE YA BEI CHEE YA VIROBA YAWAWEKA REHANI WATUMIAJI"

Back To Top