MAPOROMOKO YAUA WANNE NA WATANO WAFUKIWA NA KIFUSI UFARANSA

Watu wanne wamekufa papo hapo na watano wamefukiwa na kifusi cha barafu kusini mwa ufaransa karibu na mpaka wa italia,watu hao ambao ni wanamichezo wa maeneo ya barafu(skies) ktk milima ya Alps iliyopo nchini humo.

Maporomoko hayo yametokea jirani na hoteli ya kupumzikia watalii ktk milima hiyo ijulikanayo kam alpine resort of tignes iliwazoa watalii wapatao wanane walikuwepo eneo hilo,tukio hilo lilitokea mita zipatazo 2,100 kutoka usawa wa bahari majira ya saa nne na dakka thelathini na tano(10:35) asubuhi kwa majra ya eneo hilo.

Ukubwa wa maporomoko hayo ulikua zaidi ya mita mia nne,si mara ya kwanza kutokea kwa maporomoko ya barafu na kusababisha vifo vya watu wengi ktk maeneo hayo. juhudi za kuwaokoa walionasa chini ya vifusi hivyo zinaendelea japo uhakika wa kuwapata watu watano waliopo chini ya ardhi ni mdogo sana.

Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme

Related Post:

0 Comments "MAPOROMOKO YAUA WANNE NA WATANO WAFUKIWA NA KIFUSI UFARANSA"

Back To Top