MAMA MJANE ATUMBUA JIPU LA KUTAKA KUDHULUMIWA MALI ZAKE ZA MIRATHI

Mwanamama sabaha mohamed ally ameamua kutumbua jipu la kesi yake ya mirathi kutoka kwa mumewe baada kuhangaika san ktk sekta mbalimbli za sheria na haki zikiwemo ofisi za mawakili,vituo vya haki,polisi,mahakama za mwanzo na wilaya na kugomga mwamba.
Ndipo kufukia jana ktk kilele chqa wiki ya  mahakama ambapo raisi maguli alialikwa kama mgeni rasmi ktk sherehe hiyo.
Ilipofika mwishoni mwa sherehe  hizo ghafla aliinuka mama mtu mzima akiwa na bango la kitambaa lenye maandishi akielekea mbele kwa raisi lakini kabla kufika walinzi walimrudisha nyuma kwa nguvu sana na hapo ndipo mh.raisi alipoamua kumruhusu aje mbele na kueleza yanayomsibu,mama aliamua kutoa ya moyoni kwa kueleza jinsi anavyozungushwa kwa mda mrefu sana ktk kesi yake ya madai ya mirathi kutoka kwa marehemu mume wake,
Baada kumsikiliza kwa makini magufuli aliamuru mwanamama huyo kupewa ulinzi wa polisi na alindwe kila aendako kwakua nahofia usalama wake juu ya watu wanaotishia uhai wake kwa kuendelea kufuatilia mali hizo.
Mama amabae ni mkazi wa tanga mwenye asili ya kenya aliolewa na na mtanzania,kesi yake imeamliwa kuletwa haraka mahakama za juu na kusikilizwa haraka iwezekanavyo na kupewa haki yake.
kitendo na ujasili wa mama huyo wa kuwa tayari kwa chochote ikiwemo kuifungwa kiliwastajabisha watu wengi waliokuwepo ktk shughuli hiyo.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MAMA MJANE ATUMBUA JIPU LA KUTAKA KUDHULUMIWA MALI ZAKE ZA MIRATHI"

Back To Top