KWANINI MWANADAMU ANASAHAU?


Kusahau ni  jambo la  kawaida kwa mawanadamu yeyote yule Ila inakuwa tatizo zaidi ikiwa hali hiyo itazidi kwa kiwango kikubwa litatoka kuwa jambo la  kawaida na kuwa kama ugonjwa na kuleta madhara ktk utendaji na ufanisi wa maisha ya mtu  au kikundi cha watu.
Usahaulifu au kusahau ni hali ya mtu  kuwa na mambo au jambo fulani ambalo anakusudia kulisema au kutenda kwa mda fulani  anashindwa kuleta kumbukumbu za awali na kusabaisha kushindwa kutekeleza.
ZIFUATAZO NI SABABU ZINAZO SABABISHA KUSAHAU.
(1)Ubongo kuwa na uwezo mdogo na wa chini ktk na kushindwa kuleta kumbukumbu za awali.
(2)Mwingiliano wa taarifa nyinginkwa wakati mmoja! Mfano mtu  kusoma na   kuikiliza taarifa nyingine anazopenda.
(3)Kuwa na msongo wa mawazo na mistuko ya ghafla inasababisha mtu  kupoteza kumbukumbu za awali.
(4)Kuwa na mambo mengi kwa wakati mmoja.
(5)Kushambuliwa na magonjwa yanayoathiri mfumo wa fahamu na ubongo hasa  wakati wa utoto.
(6) Lishe zisizo zingatia viwango na aina ya vyakula kwa Afya ya mwanadamu.
(7)Kutokuwa makini na kutotia maanani ktk jambo husika.
(8)Matumizi ya vilevi na madawabya aina mbalimbali.kama pombe,cocaine.
(9)Uzalishaji wa kiwango cha chini ya homoni ya thaeroxine ktk mwili.
(10)Kupotea au kufutika kwa tukio kwa kukaa mda mrefu sana bila kulifanyia kazi au kutokea kitu kitakacho kufanya kulikumbuka.
(11)Kutokupumzika kwa wakati mwafaka.kukosa usingizi.

Ziko sababu nyingine nyingi pia nazo huchangia kuleta hali  ya usahaulifu kwa wanadamu ikiwemo kupata ajali ya kichwani,kuwa na umri mwingi au kuzeeka,kuugua magonjwa ya akili na mfumo wa fahamu kama kifafa,degedege,kiharusi,misongo ya mawazo ya kimahusiano na talaka,kuogopa,hali ngumu na mbaya ya kiuchumi.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "KWANINI MWANADAMU ANASAHAU?"

Back To Top