Mwanamuziki maarufu wa muziki wa kizazi kipya bongo flava (Diamond platinum) jana alionekana kuingia kituo cha polisi kikuu cha mjini,watu walioshuhudia kitu hicho walishangazwa sana lakini wapekuzi wa mambo walipohoji juu ya ujio wake hapo,waligundua kuwa alikwenda hapo kwa wito maalum wa mkuu wa kikosi cha barabarani Kamanda Mohamed Mpinga.Kitu kilichomfikisha ni kuhojiwa na kuonywa juu ya kuendesha gari yake kwa fujo na kutovaa mkanda wa usalama,lakini zaidi ilkuwa juu ya ukiukwaji wa kanuni na sheria za barabara kwa kuendesha kwa mwendo kasi. lakini aliachiwa mapema tu baada ya mahojiano na kulipa faini ya pesa taslimu.


0 Comments "DIAMOND PLATINUM ATINGA KITUO CHA POLISI"