
Umoja wa mataifa,ulaya na marekani waliongeza vikwazo zaidi kwa korea kaskazini na kuagiza nchi ya china kuacha mara moja ununuzi wa makaa ya mawe kutoka taifa hilo,china ndio taifa lenye uhusiano wa karibu na korea kaskazini lakini pia ndio wanafanya biashara kwa kiwango kikubwa,china ununua kiwango kikubwa cha makaa ya mawe toka nchi hiyo,hivyo usitishwaji huo utaiathiri serikali ya kim jong un kifedha.
Moja ya sababu iliyofanya china kusitisha ununuzi huo wa makaa ya mawe tokas korea kaskazini ni juu ya mauaji ya kaka wa kim jong unajulikanaye kama kim jong nam huko malyasia uwanja wa ndege.
China utumia makaa ya mawe kwa wingi kwa kuzalisha nishati ya umeme kwa ajili ya viwanda vyake.
0 Comments "CHINA YASITISHA UINGIZAJI WA MAKAA YA MAWE TOKA KOREA KASKAZINI"