BWAWA LA KUZALISHA NGUVU ZA UMEME LATISHIA UHAI WA WATU CALFORNIA

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jimbo la calfornia huko nchini marekani zimeleta balaa kwa kujaza kiwango kikubwa cha maji ktk bwawa la kuzalisha nguvu za umeme lijulikanalo kama (Oroville dam) lililopo jimbo la calfornia magharibi.

Bwawa hilo limeanza kuonekana hatari baada ya kupasua kingo za kuta za bwawa hilo na maji kuelekea ktk maeneo ya makazi ya watu,viongozi wa jimbo hilo hasa ktk miji ya (butte,yuba,marysville) yalipo ktk jimbo hilo la calfornia wamewatahadharisha wananchi kuhama na kwenda maeneo mengine ambayo ni salama kwa maisha yao na sio kukaa hapo kwa kuna dalili za msingi wa mvua kuendelea zaidi na kuweza kufanya bwawa kupasuka na kuleta madhara makubwa.

Idadi ya watu zaidi ya laki moja themanini na nane elfu((188,000) kati ya laki mbili(200000) wanaotakiwa kuhama wameshahama kutoka maeneo hayo .

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "BWAWA LA KUZALISHA NGUVU ZA UMEME LATISHIA UHAI WA WATU CALFORNIA"

Back To Top