BOSI WA KUNDI LA YAKUZA JAPAN AKAMATWA NA KURUDISHWA TENA JELA

Kiongozi wa kundi kimafia na kibabe la japani lijulikanalo kama Yakuza amekamatwa upya tena kwa mara pili na kurudihswa jela,boss huyu anaejulikana kama Yoshiyuki takayama  alishahukumiwa kukaa jela miaka minane kwa makosa ya kujipatia mali kwa njia siziso hali ambazo ni za kibabe kama kutumia nguvu,silaha na vitisho kwa watu.

Baada ya kuhukumiwa kifungo hiko mwaka 2010  mwaka huu aliita timu ya madaktari ili kumuangalia afya yake na ndipo madaktari walipotoa ripoti kuw afya ya takayama ni dhaifu sana hivyo si vyema endapo ataendelea kukaa jela kwani anaweza kupoteza uhai.

Baada ya ripoti hiyo takayama aliachiwa na kupata kifungo cha nnje kwa mda lakini timu ya madaktari wengine walipomchunguza kwa kina waligundua kuwa takayama haumwi kwa kiasi hiko hivyo ni mbinu za hila ambazo zilitumika ili kumtoa kiongozi huyo nje.takayama alikamtwa na kurudishwa jela kuendelea na kifungo chake.

Magenge haya ya kihalifu yamesumbua sana serikali ya japani toka miaka ya 1980 kwa kuongoza kufanya mambo ya kihuni,mauji,uporaji,ubakaji na kila aina ya mambo mabaya.

Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme

Related Post:

0 Comments "BOSI WA KUNDI LA YAKUZA JAPAN AKAMATWA NA KURUDISHWA TENA JELA"

Back To Top