BIASHARA YA MAFANIKIO!

 Biashara ni shughuli yeyote ile ambayo mtu anaifanya kwa kusudio la kupata faida au kipato(fedha) kwa kusudio la kuendesha maisha yake ya kila siku,kwa maana hiyo biashara ziko za aina nyingi sana,mfano biashara ktk mawasiliano,usafirishaji,elimu,bidhaa mbalimbali za vyakula na vinywaji,vifaa za ujenzi,umeme,magari,nguo n.k,biashara ziko kubwa na ndogo nikiwa na maana za ukubwa wa mtaji wa hiyo biashara,kila mmoja ana nafasi ya kuanzisha biashara kulingana na eneo na mtaji wa mtu alionao! Watu Wengi huanzisha biashara nyingi sana Ila wanajikuta zinakufa baada ya muda mfupi sana! Sasa tujaribu kuangazia maswala ambayo mtu anapaswa kufanya ili aweze kudumu,kuendelea na kutengeneza faida zaidi ikiwemo na mtaji wake kukua kadri siku zinavyokwenda! Kwakua tuna mifano ya makampuni makubwa huko ulaya,Asia na marekani ambayo yalianzishwa kama biashara ndogo na mtu au kikundi cha watu kwa mfano cocacola,Toyota,Microsoft,apple,mc Donalds,shoprite,uchumi supermarket,azam group,mo industries n.k.Je ni mbinu zipi zinazotumika kuwezesha biashara kukua,kuendelea na Image may contain: food faida kubwa kama ilivyokusudiwa na muazishaji wa biashara hiyo?

MBINU ZITUMIKAZO KTK BIASHARA:-Mambo muhimu ambayo mtu anapaswa kuyafuata kabla na baada ya kuanzisha biashara ni...Kufanya biashara unayoendana nayo ikiwa na maana ya kuwa na ujuzi nayo,kupata maelekezo kutoka kwa wataalam au watu wanayoifanya biashara hiyo kabla yako,kuandaa (business plan) mtirirko wa biashara ikiwemo gharama za mt
aji,manunuzi,vifaa unavyotakiwa kuwa navyo,kodi na gharama za biashara ktk jengo,kujua kama italeta faida au hasara matazamio,kujua na kufanya utafiti juubya soko au idadi ya wateja juu ya biashara hiyo,kuitangaza biashara yako ktk vyombo vya habari inapobidi,kuangalia mahitaji ya watu ktk biadhaa na aina ya biashara,kuchagua eneo zuri lililo na wateja wa bidhaa yako(location),kuweka biashara eneo salama kutokana wizi,majanga ya mafuriko,moto,wadudu waharibifu,kupata vibalo na ruhusa kutoka serikalini,Note kuendelea kwa biashara yako kukupa faida kubwa utegemea sana na ubunifu wa mfanyabishara na muuzaji husika,vitu kama kauli zako juu wateja wako inaweza kuwa kivutio au kuwakimbiza wateja,ni muhimu sana kuwajali wateja kwa asilimia zote kwani hao ndio mabosi zako wakuu,jitahidi kutomkera au kumbughuzi mteja wako kwa hali yeyote ya kawaida yakupasa kumvumilia,watu Wengi wamejikuta wakipoteza soko(wateja) kwa matendo yao na maneno,uchafu wa mazingira na muuzaji,kutokujali muda wa kufungua na kufunga biashara,kukosekana kwa baadhi ya bidhaa muhimu nyakati nyingi,ucheleweshaji ktk kuhudumia wateja,kukosa chenji,kuuza bidhaa zilizokwisha wakati!! Mungu atubariki ktk biashara zetu!

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "BIASHARA YA MAFANIKIO! "

Back To Top