Wananchi wa afrika ya kusini wameamua kuingia barabarani kwa Mara ya pili kupinga uwepo wa wahamaji Wengi wanaozidi kufulika nchini humo kutoka mataifa ya mbali na jirani.
Ikumbukwe hii ni Mara ya pili kwa waafrika kusini kufanya matukio haya ya kuandamana juu ya kupinga uingiaji na uwepo wa wageni ndani ya nchi yao,miaka michache nyuma waliandamana na kuwapiga vibaya wahamiaji kutoka Zimbabwe waliokimbia hali ngumu ya uchumi iliyotokana na mfumuko wa bei na kwenda nchini humo kwa ajili ya kutafuta kazi.
Maandamano hayo yanakuja baada ya malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya kukosekana kwa ajira miongoni mwa wazawa wa nchi hiyo inayotokana na ujio mkubwa wa wahamiaji kutok mataifa wa afrika.
Waandamanaji walionekana wakishika silaha kam mapanga,shoka,nyundo na magongo wakiashiria kutaka kuwapiga wahamiaji.
Rais wa afrika kusini Jacob Zuma amewasihi raia zake juu ya kuwa watulivu na kutunza amani ya taifa lao.
0 Comments "AFRIKA YA KUSINI NAO WAJA JUU DHIDI YA WAHAMIAJI"