
Watu hao walikuwa wakiandamana wakiwa wamebeba mabango yenye maneno yanayshinikiza kwa kiongozi aliyekuwepo madarakani kupanga tarehe ya uchaguzi rasmi. fujo hizi zinaibuka wakati wiki mbili zilizopita wapinzani wametoka kumpoteza kiongozi wao shupavu Ettiene Tshikedi aliyefariki akiwa katika matibabu nchini ubeligiji.
Kifo cha kiongozi huyo kimeleta taharuki na sitomfahamu kwa wananchi wakliokuwa na matumaini na kiongozi wao kuwapeleka ktk uchaguzi mkuu ujao.
Zaidi ya watu ishirini na sita (26) wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi waliokua maeneo ya tukio hasa ktk mji mkuu wa kinshasa wakiamndamana kupinga uwepo wa Rais joseph kabila.
Congo ni miongoni mwa taifa tajiri kwa madini ya aina nyingi,rasilimali za misitu na eneo kubwa la kilimo lakini taifa hili linakumbwa na machafuko ya wenyewe kwa wenyewe kwa mda mrefu toka kuuawa kwa aliyekuwa waziri mkuu Patrice lumumba wa congo miaka 1960 na kutawaliwa kidikteta na Mobutu sese seko,Laurent disire kabila.
Asi;limia kubwa ya wakazi wa nchi hii wamekimbilia nchi za jirani kama Tanzania kulinda uhai wao.
0 Comments "26 WAUAWA KTK MAANDAMANO CONGO DRC"