MWANASHERIA MKUU WA MAREKANI ATIMULIWA KAZI

Raisi wa marekani amemfukuza kazi mwanasheria Mkuu wa nchi hiyo baada kupinga na kubeza agizo lake.
Trump anaejulikana kwa misimamo yake thabiti kabla na hata baada ya kupata cheo hicho cha ngazi ya juu,alisistiza juu ya kuweka sheria kali ya uhamiaji itakayo dhibiti wahamiaji haramu na kupunguza idadi ya wageni  ndani ya nchi hiyo.
Sheria hii inakuja baada ya kuibuka kwa wimbi la matukio  ugaidi hasa kutoka nchi za mashariki ya kati,pia swala la  wahamiji kutoka nchi zenye machafuko ya vita,njaa kama Iraq,syria,afghanstan,Congo DRC,somalia kukimbilia ulaya na marekani.
Mwanasheria Sally Yates ambae aliteulewa utawala uliopita wa raisi Obama alifukuzwa Jana mapema baada yankuonekana akipinga waziwazi uamuzi wa trump juu ya kufungia nchi saba na kurekebisha sheria hiyo ili iweze kubana zaidi.
Sally alionekana kupinga amri hiyo na kuikosoa kwa udhaifu wake na hata kuhisi inaweza kuleta machafuko hapo baade.


Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MWANASHERIA MKUU WA MAREKANI ATIMULIWA KAZI"

Back To Top