JE WAJUA! KUWA VIFAA VINGI VYA UMEME UHARIBIKA KABLA YA WAKATI WAKE KUTOKANA NA KUTOKUJUA JINSI YA KUVITUMIA KAMA INAVYOHITAJIKA!



 Si jambo la ajabu sana kuona unaweza kununua kifaa cha umeme leo na pindi unapotaka kutumia tu ukakuta hakifanyi kazi au ukatumia kwa muda mchache sana na kikaharibika!!
Yako makosa yanayosababishwa na udhaifu ktk kutengenezwa kwake,lakini asilimia 98% ya kuaharibika kwa vifaa hivi hutokana na matumizi mabaya na kutofuata masharti ya kifaa husika.
Vifaa kama runinga,feni,kiyoyozi,radio,Paso,kompyutan.k kila kimoja kina maelekezo maalum jinsi gani unaweza kukitunia na kuleta ufanisi,kidumu pia kisilete madhara kwa mtumiaji au Mali ya mtumiaji wa kifaa hiko.
Kila mmoja wetu anafahamu fika kuwa umeme ni mzuri,muhimu na unaleta maendeleo na maisha ya kisasa ktk jamii na hata kurahisisha maisha na utendaji kazi wetu ktk shughuli mbalimbali.
Lakini ni nani asiyejua madhara yatokanayo na matumizi mabaya ya umeme ikiwemo kuharibu kifaa husika,kuua,kuunguza Mali kama nyumba,vyombo na hata kuleta ulemavu wa kudumu kwa atakaathirika na umeme huo.
Kwa hivyo inanahitajika kuutumia umeme kwa umakini wetu wote,hasa vifaa vutumiavyo umeme vitumiwe na mtu mkubwa mwenye ujuzi,kujitambua angalau miaka 18 na kuendelea.
Kununua vifaa imara,kuweka miundombinubya umeme hasa ndani ktk hali ya usalama kabisa.

ZIFUATAZO NI NJIA ZA KUFANYA VIFAA VYAKO VITUMIKE KWA USALAMA NA KUFANYA VIDUMU KWA MUDA MREFU ZAIDI:-
(1)Tazama kwa makini sana kifaa ulichionunua kinatumia kiasi au aina gani ya umeme kama ni AC 100/110/220/240 VOLTAGE au DC 1-12-24 VOLTAGE.
(2)Nunua kifaa chako ktk kampuni ktk kampuni inayoamika kwa kutengeneza vifaa imara duniani au nchini(original or guniune) kama general electric,Samsung n.k.
(3)Hakikisha kifaa kina warranty au matamazio kwa mda Fulani ktk matumizi yake.
(4)Hakikisha unanunua kifaa kilicho na kitabu cha maelekezo ya jinsi ya kutumia kifaa hiko(MANUAL BOOK) na kabla ya kuanza kutumia hakikiasha unakisoma kwa makini sana na wala usikitupe daima.
(5)Hakikisha unakitumia kifaa hiko ktk mazingira salama yalio na hewa ya safi ya kutosha,yasiyo na unyevu wala maji wala unyevu,vumbi kwani vifaa vingi vya umeme huathirika sana na hata kuaharibik endapo vitatumika ktk mazingira ya aina hii.
(6)Tumia kifaa hiko kwa matumizi sahihi kama ikivyelekezwa(uzito wa mzigo) maximum load,msaa ya kufanya kazi.usizidishe mzigo kupita maekekezo.
(7)Endapo kitapata matatizo yeyote basi usikifungue wa kuhangaika nacho,inatakiwa kukipeleka kwa wataalam na kubadili vifaa origino endapo itahitajika kufanya hivyo.
(8)Tumia vifaa vya kuzui mwenendo wa umeme kama(regulator,stabilizer,circuit breaker,main switch,ups) ili kuzuia kifaa kisingue au kuharibika endapo tatizo lolote la umeme kuzidi au kupungua.
(9)Hakikiasha au pendelea sana kununua vifaa vipya(new) na sio vya zamani au vilivyotumika(old or used).
(10)Kutumia vifaa vya umeme na kuwepo eneo husika,vifaa vingi vinahitajika utumie nawe ukiwepo kama feni,runinga,pasi,jiko,radio kasoro fridge n.k,ni hatari kutumia kifaa wakati wewe haupo kwani kifaa kama pasi,jiko,heater huweza kushika moto na kuleta madhara makubwa kwa Mali zako.
(11) Kuzuma swichi zote endapo utakuwa unakusudia kuondoka ktk eneo nyumbani.kuepusha hatari za moto.
(12)Kutoruhusu na kuweka mbali kabisa vifaa vya umeme na watoto,watu wenye matatizo ya akili wala kutowaruhusu kutumia vifaa hivyo.
(13)Kutumia swith au sakiti kulingana na uwezo wa kifaa unachotaka kutumia,mfano jiko la umeme hutumia umeme mwingi sana na wenye nguvu usiofanana na umeme wa runinga,hivyo njia zake hutofautiana kabisa.
(14)Kuichunguza kila Mara miundombinu ya umeme ndani ya nyumba yako ili kuzuia nyaya zilizowazi kuzuia shoti.
(15)Kusafisha kifaa au kwenda kukifanyia service kifaa kama kilivyoelekezwa ktk kitabu chako,ikiwa kusafisha au kuripea.
Kumbuka umeme ni hatari sana kwa maisha hata Mali zako,hivyo unahitajika kuwa makini kwa uwezo wako wote ktk kuutumia umeme,usikubali kwenda kununua vifaa feki,jitahidi kutumia kwa makini sana,na hapo utajikuta unatumia kifaa kwa muda mrefu sana bila kuharibika.

(IMEANDIKWA NA H.S WOGOLE)

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "JE WAJUA! KUWA VIFAA VINGI VYA UMEME UHARIBIKA KABLA YA WAKATI WAKE KUTOKANA NA KUTOKUJUA JINSI YA KUVITUMIA KAMA INAVYOHITAJIKA! "

Back To Top