MTWARA YAJIVUA NA AIBU YA KUWA NA SHULE ZA MWISHO KITAIFA

  


Hatimae mkoa wa mtwara umejivua na aibu ya kuwa mingoni mwa mkoa wenye kufanya vibaya kitaifa hasa  kwa mwaka 2016 na mwanzoni mwaka huu 2017 ktk matokeo ya shule za msingi darasa la saba na kdato cha pili.
Matokeo ya darasa la saba yalipotoka mwezi novemba yalikua mabaya haa kwa wilaya za mtwara vijijini,nanyumbu,Tandahimba na newala na ikalazimika Afisa elimu mkoa kutoa maagizo ya kushushwa vyeo kwa wakuu wote  wa shule zilizofelisha.
Hali hiyo pia imejirudia tena mwaka 2017 mwezi January ktk matokeo ya kidato cha pili na darasa nne  kwa shule za msingi ambayo yalikua mabaya zaidi na kupelekea kuwa na shule tisa kati ya kumi za mwisho kitaifa.
Hii ikapelekea serikali kutolea macho mkoa  huu kwa jicho la  karibu zaidi na kusababisha waziri Mkuu kutuma timu ya wataalam wa elimu kuja kufanya uchunguzi zaidi juu ya matokeo hayo mabaya.
Kufikia leo  31/1/2017 matokeo ya kiadato cha nne  yalitangazwa na kuonekana mkoa wa mtwara haupo tena ktk shule kumi za mwishi,safari hi shule sita(6) za mwishi kitaifa zimetoka mkoa wa Dar es salaam,lindi 1,pwani 1,kilimanjaro 1 na mkoa arusha pia moja.
Hatua hii ya kutokuwepo kwa mkoa wa mtwara ktk shule za mwisho inaleta matumani mapya juu mtazamo w elimu kwa wanafunzi,walimu,serikali,jamii na wadau wa elimu kutokana na sintofahamu iliyojitokeza kwa matokeo ya hapo nyuma na kusababisha kila mmoja kutupa lawama kwa mwenzie na mwisho wa Siku mwalimu ndio alikua wa kwanza kupata lawama hizo kwakua yeye ndie anayehusika ktk swala zima la  kufundisha na kuelekeza mwanafunzi.



Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comments "MTWARA YAJIVUA NA AIBU YA KUWA NA SHULE ZA MWISHO KITAIFA"

Back To Top